KYUNGA AZIAGIZA HALMASHAURI KUTANGAZA VIVUTIO KWA WAWEKEZAJI GEITA

Share it:
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza  kwenye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.
Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akitoa maelekezo na ushauri.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Nicas Mayala akisisitiza kufanyia kazi ushauri ambao wamepatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Mkurugenzi wa NGM GOLD MINE Emmanuel Gungu Siganga akipokea cheti cha Pongezi Kutoka kwa mmwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kwa kuwa mdau mkubwa  wa kuchangia maendeleo kwenye sekta mbali mbali Wilayani Humo.

Baadhi ya wakuu wa Idara wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani Wilayani Bukombe.



 PICHA NA JOEL MADUKA



Halmashauri zilizopo Mkoani Geita,zimetakiwa Kutangaza Vivutio ambavyo vitaweza kuwavutia wawekezaji  ili waweze kuwekeza kwenye Maeneo yao.

Rai hiyo ameitoa Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kwenye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya  Bukombe .

Ambapo amesema kuwa Halmashauri Nyingi ikiwemo ya Bukombe ina maeneo mengi ambayo yanauwezo wa kuwavutia wawekezaji tatizo kubwa ni kutokutangaza fursa hizo.

“Kwasababu mwenye macho aambiwi tazama sisi wote jamani tunaona kwenye Vyombo vya habari namna halmashauri mbali mbali zinavyochachalika kutangaza Fursa zao halmashauri unakuta imejiwekea utaratibu inatangaza yenyewe fursa inaita wawekezaji mbali mbali jamani ninachotaka kusema tuchachalike fursa tunazo na tuzitangaze tuone ni wapi ambapo tunaweza kupata wawekezaji”Alisisitiza  Kyunga.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe,Nicas Mayala amemwakikishia Mkuu wa mkoa kuanza kufanyia kazi maelekezo na ushauri ambao ameutoa kwenye Halmashauri Hiyo huku akiwataka wawekezaji kuja kuwekeza Bukombe kutoka na na kuwepo kwa mifugo mingi ya Ng’ombe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Hiyo,Dionis Myinga amehaidi kufuatilia na kutafuta wawekezaji ambao wataweza kuwekeza kwenye Wilaya Hiyo na kwamba  bado kunafursa nyingi za uwekezaji .

Hatua hiyo imekuja ni kutokana na halmashauri  hiyo ,Mkoani Hapa Kuwa na Idadi Kubwa ya Mifugo ikiwemo Ng’ombe.



IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Share it:

habari

Post A Comment: