VIJANA WAMETAKIWA KUTUMIA KILIMO CHA GREEN HOUSE KUJIAJIRI GEITA

Share it:
Kiongozi wa Mbio za  Mwenge wa uhueu Kitaifa,Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi wakati wa kukimbiza mbio za mwenge kwenye Wilaya ya Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi.

Mwenge wa Uhuru ukipitishwa kwenye kamati ya Ulinzi na usalama Wilayani Geita.

Mwenge wa Uhuru ukipitishwa kwa viongozi wa Dini na madhahebu mbali mbali Wilayani Geita.

Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lorencian Bukwimba akizungumza na kutoa salaam Kwa wananchi wa kijiji Nyachiruruma.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru akiweka Jiwa la Msingi kwenye Kituo cha afya cha Inyara.

Vitanda ambavyo vimo kwenye kituo hicho.

Mradi wa Green House ambao unasimamiwa na kikundi cha viajana wa Busanda.

Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Wilaya na Mkoa wa Geita wakitembelea Mradi wa Kilimo cha Green House.

Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa,akimpongeza Diwani wa Kata ya Busanda Elias Kisome kwa shughuli ya kuwajengea vijana uwezo wa kulima kilimo hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi pamoja na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Thomas Dimme wakimsikiliza Kiongozi wa Mwenge wa uhuru Taifa.

Vijana wametakiwa  kujiajili kwa kuunda vikundi ambavyo vinaweza kuwasaidia kupatiwa Mkopo kutoka kwenye Halmashauri ambazo wanaishi.

Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour wakati alipokagua kikundi cha vijana ambao wanajishughulisha na kilimo cha Green House Kwenye kata ya Busanda Wilayani Geita.

Amesema kuwa Vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo ni vyema wakawezeshwa kwa Mikopo ikiwa ni pamoja na kufuatiliwa kwa kina miradi ambayo wanakuwa wameianzisha.

Pia ameongeza kuwa kukaa pamoja ni jambo ambalo linaweza kuchukua muda lakini ni jambo zuri kwani palipo na umoja kuna nguvu kubwa ya mafanikio.

“Hatuitaji viongozi ambao hawapo tayari kuwasaidia wananchi nyie niwapongezeni nakijua kilimo cha green house nina amini kuwa mtapata faida kwa kile ambacho mmekitumia kinaweza kurudi mala mbili zaidi”Alisema Hamad

Japhet Msuka,ameeleza kuwa kilimo ambacho wamekuwa wakikifanya kimeweza kuwaletea maendeleo ya vipato vya kuendeleza maisha pamoja na kukidhi haja zao.

Hata hivyo Kiongozi wa mbio za Mwenge Amour Hamad Amour pamoja na Kuwapongeza wanakikundi hicho ambacho kinavijana Arobaini na Mbili pia amempongeza Diwani wa kata hiyo,  Elias Kisome kwa juhudi ambazo amezifanya hadi kufikia hatua ya kuwakusanya vijana na kuwapa mbinu ya kubuni mradi huo.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Share it:

habari

Post A Comment: