MBUNGE MSUKUMA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI GEITA

Share it:
Mbunge wa Jimbo la Geita ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoani Geita ,Joseph Kasheku Msukuma akizungumza na wananchi m jimboni kwake(PICHA NI KUTOKA MAKTABA YA MADUKA ONLINE).

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo Akizungumza na waandishi wa Habari juu ya tukio la kuandamana wa madiwani wa Halmashauri mbili za Mji na Wilaya.


Jeshi la polisi Mkoani Geita linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Geita  Joseph Kasheku Msukuma kutokana na tukio la maadamano ambayo yalifanyika siku ya Alhamisi wiki hii yaliyopelekea uharibifu wa  miundombinu ya maji kwenye mgodi huo.

Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo amezungumza na Maduka online  ambapo amesema kuwa wanawashikilia madiwani sita  pamoja na mbunge huyo kwaajili ya kufanya nao mahojiano ambayo yatabaini ni wakina nani ambao wamehusika na tukio hilo la kuandamana  kinyume na sheria.

Amesema kuwa Mbunge huyo wamemkamata majira ya mchana mjini Geita na kwamba wanaendelea na mahojiano  ambayo yatasaidia kuwabaini wale ambao walihusika na tukio.

Kamanda Mponjoli amesema jeshi lake linaendelea na msako wa kuwabaini,kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wahusika wa  tukio hilo na kwamba sheria ya makosa ya jinai hayana  kikomo na kwamba  mtu akifanya kosa leo na akakwepa ataendelea kutafutwa,na hana namna ya kuukwepa  Mkono wa sheria.


 Mapema wiki  hii  ,jeshi hilo lililazimika kutumia nguvu kutawanya maandamano ya madiwani pamoja na wananchi walioweka vizuizi katika barabara inayoingia mgodini wakishinikiza kulipwa ushuru wa huduma kiasi cha dola za kimarekani milioni 12.65 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 26.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

Share it:

matukio

Post A Comment: