Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January
Makamba akifanya mahojiano maalumu katika Kituo cha Redio cha Cocunut FM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January
Makamba ameanza ziara ya kikazi ya siku saba visiwani Zanzibar. Katika siku ya
kwanza Mhe. Makamba amepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya
ya Wafanyabiashara wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kubaini fursa
na changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kupata ufumbuzi.
Miongoni mwa changamoto
zilizojadiliwa na kuwekewa mikakati ya utekelezaji ni pamoja na masuala ya
kodi, namna ya kunufaika kutoka na fursa zilizopo baina ya pande zote mbili za
Muungano na kuondoa vikwazo vinavyotokana na changamoto hizo ili kuleta
ufanisi.
Mhe. Makamba amewahakikishia wana
juimuiya hao kuwa Ofisi yake itaratibu vikao kati ya Ofisi yake na
wafanyabiashara hao ili kupata fursa ya kutoa mrejesho wa utekelezaji wa mambo
waliyokubaliana.
Mbali ya kukutana na wafanyabiashara
hao Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Vyombo mbalimbali vya Habari
hapa Unguja kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Muungano. Vyombo
vilivyotembelewa ni pamoja na Zenji FM na Zenji Tv, Bahari FM na Cocunut FM.
Ziara ya Waziri Makamba katika siku
pili atatembelea Miradi mikubwa ya Mazingira na kuwa na Vikao na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB).
|
Post A Comment: