MWANAMKE AMLILIA RAIS MAGUFULI KWA MADAI AMEVUNJIWA NYUMBA YAKE SENGEREMA

Share it:
Rais John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela kuyafanyia kazi malalamiko ya mwanamke mmoja mkazi wa Sengerema aliyedai kunyanyaswa na kuvunjiwa nyumba yake.

Rais ametoa agizo hilo leo (Jumanne Julai 4) wakati akizindua mradi wa maji, wilayani Sengerema na kumtaka Mongela kuchukua namba ya simu ya mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rosemary Simon, ili atatuliwe tatizo lake.

 Kabla ya Rais Magufuli kuchukua hatua hiyo, mwanamke huyo alikwenda mbele ya jukwaa alimoketi Rais, huku akilia kuwa ananyanyaswa na viongozi wa Chadema na kuwa wanataka kumbomolea nyumba yake, bila kufafanua ni kwa vipi.

“Mpe simu yako Mkuu wa Mkoa, halafu atakutafuta na wala usijali, nitamtuma Mkuu wa Mkoa  na haki yako itatendeka, nitalifanyia kazi suala lako,” amesema Rais.
Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

ROSE BONANZA AFUNGUKA KUHUSU MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA DHAHABU GEITA

JOEL MADUKA