MACHINGA WAPATA UHURU KUTOKANA NA AGIZO LA RAIS

Share it:






Moshi.  Mbunge wa Moshi Mjini, Jafary Michael (Chadema) amempongeza Rais John  Magufuli kwa kuwaruhusu wafanyabiashara ndogondogo, wamachinga kuendelea kufanya biashara zao bila ya kubughudhiwa.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Manispaa ya Moshi jana, alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza makundi mabaya ndani ya jamii.

Michael alisema siku zote amekuwa  akiwapigania wafanyabiashara hao na kuwawekea mazingira rafiki kwa ajili ya biashara zao lakini walikuwa wakisumbuliwa, hivyo kauli ya Rais itawafanya wawe huru
Share it:

habari

Post A Comment: