Samaki hao walikuwa wakiingizwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa, kinyume cha sheria.
Walikamatwa juzi katika operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu.
Samaki hao walikuwa wanasambazwa kwenye masoko ya Nyankumbu, Shilabela na Soko la mjini Geita.
Ofisa Mfawidhi mdhibiti ubora wa samaki na msimamizi wa raslimali za uvuvi, Shafii Kitery alisema samaki hao walikamatwa kunatokana na taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Alisema wananchi hao walieleza kuwapo wafanyabiashara waliokuwa wakivua
samaki wachanga chini ya sentimita 50 hivyo ukawekwa mtego na
kuwakamata.
“Ninashukuru ushirikiano wa wananchi ambao wametoa taarifa hizi, Hii ni hatua endelevu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli
alilolitoa Mwanza akitaka kupambana na uvuvi haramu na kuwalinda samaki
wachanga,Masoko yote Geita tutayafanyia uchunguzi na kuhakikisha hawa samaki wachanga hawauzwi,Watu wanane tuliowakamata tunawafikisha kwenye vyombo vya sheria vichukue mkondo wake,” alisema Kitery.
Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amekuwa na oparesheni ya kuzunguka kwenye visiwa vilivyopo wilayani humo ambavyo ni izumacheli na Nkome lengo likiwa ni kuzungumza na wananchi na kuwaimiza kuachana na tabia ya uvuvi haramu ambao umeendelea kusababisha samaki wengi kutoweka katika ziwa victoria .
Post A Comment: