CCM WILAYA YA GEITA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI.

Share it:
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha mapinduzi Wilayani Geita wakiwa kwenye Mkutano wa kupitisha wagombea wa nyadhifa mbali mbali ndani ya chama.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Geita Barnabasi Mapande akiwasikiliza wajumbe ambao walikuwa wakizungumza kwenye Mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya wa Wilaya ya Geita,alivaa kahunda Suti ,Pamoja na Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho ambaye yupo katikati.

Diwani wa Kata ya Kasamwa ,Merry Kasanda akichagia hoja iliyokuwa mezani kwenye Mkutano huo

Wajumbe wakifuatilia Kikao hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola akisisitiza wananchi kuendelea kumuunga Mkono Rais wa Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Geita akiwataka wananchama kuwa mstali wa mbele kujitoa kwenye swala la maendeleo katika kuchangia michango ambayo itawezesha shughuli za kimaendeleo.

Katibu  Mwenezi wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita,Jonathan Masele akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama cha mapinduzi.

Chama cha mapinduzi CCM Wilayani Geita kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Jitihada ambazo ameendelea kuzifanya ikiwa ni pamoja na kufichua uovu kwa baadhi ya sekta za serikalini pamoja na watumishi ambao wameendelea kuhujumu uchumi wa nchi bila ya kuwa na sifa za kazi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini Kwake ,Katibu wa siasa na uenezi  wa Chama hicho Wilaya humo Jonathani Masele ,amesema kuwa shughuli na jitihada ambazo zimeendelea kufanywa na Rais Magufuli sio za kubezwa na Watanzania kwani ni muda mrefu watu wamekuwa wakijifanyia mambo na kujinufaisha Bila ya kuangalia manufaa ya Nchi.

“Tunatambua kazi ambazo anazifanya Mheshimiwa Rais sio za kubezwa kabisa kama ambavyo tumeona miaka mingi Migodi ilikuwa ikisafirisha mchanga bila hata ya watanzania kujua lakini yeye amefichua yote ambayo yalikuwa yanaendelea Mimi namuomba Rais aangalie kwa wachimbaji wadogo kwani baadhi yao wamekuwa na tabia ya kujibinafisisha maeneo mwisho wa siku wanabadilisha majina bila hata ya kuyatumia maeneo hayo na ni vyema wakanyangwanywa ili wapatiwe wale ambao wana uwezo wa kuendelea kuyatumia”Alisema Masele.

Mwenyekiti wa  Wilaya Hiyo ,Barnabas Mapande akizungumza kwenye Kikao cha Halmshauri ya Wilaya ya chama hicho  amemtaka Rais kutokuwasikiliza wale ambao wamekuwa wakimlalamikia na kwenda mbele zaidi ya Hapo ambapo amefikia.

“Ni miaka mingi Watanzania wemeahangaika kwenye sekta nyingi zikiwemo za afya na elimu lakini kwa sasa tunaamini kuwa mambo haya yote yanakwenda kufanyiwa ufumbuzi kwa haraka zaidi mimi napenda kumshauri Rais wangu aendelee na kazi ambayo anaifanya kwani ni nzuri kwa Watanzania wenye hali ya chini”Alisema Mapande.

Mkuu wa Wilaya ya Geita  Mwl Herman Kapufi ambaye ni mmoja kati ya wajumbe wa kikao hicho amewasisitiza wajumbe na wanachama kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia kwenye maswala ya elimu pamoja na afya huku akisisitiza kuwa yeye kama mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani humo atahakikisha kuwa Mgodi ambao upo kwenye Wilaya ambayo anaiongoza kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wanasimamia kwa umakini dhahabu ambazo zinasafirishwa kwenda nje ya nchi.


Kamati ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM imekutana leo lengo likiwa ni kujiandaa na uchaguzi ambao unatarajia kufanyika ndani ya chama hicho.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.



Share it:

SIASA

Post A Comment: