Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya NHIF umezindua mpango wa madaktari Bingwa Mkoani Geita lengo likiwa ni kushirikiana na serikali kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za kibingwa na kusogeza huduma karibu na wananchi pamoja na wanachama wa mfuko huo.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba amesema watu elfu kumi na tatu mia moja na sitini na saba (13167) na kati ya hao mia nne sitini(460) wamekwisha kufanyiwa huduma ya upasuaji.
“Kabla ya kuleta madaktari bingwa kwenye Mkoa husika mfuko huwa unafanya tathimini na kubaini uhitaji katika kila Mkoa ndivyo hivyo tumefanya kwenye Mkoa huu wa Geita na kuamua kuleta madaktari bingwa kama ambavyo nimeeleza kwa hiyo Tumekuja na madaktari Bingwa pamoja na Dawa na mashuka ambavyo vitasaidia kwenye huduma za kiafya”Alisema Mramba.
Aidha Bi, Mramba ameongezea kuwa matarajio ya mfuko huo ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali za ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa madaktari kutoa huduma kwa uhakika zaidi kwa watu wachache watakaolazimika kufuata huduma hizo kwenye hospitali Kubwa ikiwa ni pamoja na watumishi wa Hospitali husika kutumia fursa ya kujifunza kwa kupata ujunzi na utaalamu kupitia kwa madaktari wageni.
Kwa Upande Wake Mgeni Rasmi Ambaye ni Katibu Tawala Mkoani Humo Celestine Gesimba amewata madaktari kuwatumia madaktari bingwa waliofika Hospitalini hapo kutoa huduma kwa wagonjwa ili kujifunza mbinu mpya za utoaji wa huduma badala ya kwenda kufuata mbinu hizo nje ya maeneo yao ya kazi
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando Dr Neema Chami amesema tangu kuanza kwa huduma hizo kwa siku 2 sasa wamewahudumia watoto 80 hali inayoonesha mafanikio ya lengo la wao kufika mkoani humo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita Dr Brian Mawala amesema ombi la Wananchi la kutaka Madaktari Bingwa wawe wanafika mara kwa mara Hospitalini hapo, litafanyiwa kazi kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF ili kupunguza wananchi wasisafiri umbali mrefu kufuata huduma za Kibingwa
Zoezi la utoaji wa huduma za upasuaji kutoka kwa Madaktari Bingwa kwenye Mikoa ya Geita na Kigoma lilianza rasmi Mei 22 siku ya jumatatu kwa uratibu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF ambapo hadi sasa ni jumla ya wagonjwa 1,204 wamekwisha hudumiwa kwa siku mbili huku wagonjwa ambao wamefanyiwa upasuaji kwa mikoa miwili ni kumi na nne.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: