Wajumbe wakifuatilia hotuba ya Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma Dr,Beatrice Mutayoba wakati wa kikao hicho |
Mwakilishi wa mganga mfawidhi wa hospital ya Mkoa huo ambaye pia ni katibu,Sashisha mafuwe akielezea tatizo la kifua kikuu ambavyo lilivyo kwenye mkoa wa Geita. |
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Huo ambaye pia ni Msaidizi wa katibu Tawala Mkoani Humo.Emmily Kasagara akiwataka wajumbe kutumia kikao hicho kujadili namna ambavyo wataweza kupambana na ugonjwa huo |
Imebainika
kuwa maeneo ambayo kunafanyika shughuli za uchimbaji bado kuna tatizo kubwa la
maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu ni kutokana na kuwepo kwa msongamano
mkubwa wa watu ambao wanafanya shughuli hizo.
Hayo
yamebainishwa na Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma Dr,Beatrice Mutayoba wakati wa kikao ambacho kimewakutanisha wadau mbali mbali wakiwemo wa sekta ya afya na madini Mkoani Geita.
Amesema kuwa
pamoja na tatizo la kifua kikuu kuwa juu bado kunatatizo kubwa la uelewa kwa
watu wanaishi kwenye machimbo pamoja na wahudumu wa afya ambao wapo kwenye maeneo hayo.
“Pamoja na
jitihada ambazo zinaendelea lakini bado tunaona changamoto kubwa ni elimu
tumefika kijiji kimoja tukamuuliza muhudumu wa afya je unaelewa dalili za kifua
kikuu anasema dalili moja wapo ni mtu kutokwa na mkojo mwingi hivyo tumeona
sisi ni tatizo kubwa sana”Alisema Mutayoba.
Aidha mwakilishi wa mganga mfawidhi wa hospital ya
Mkoa huo ambaye pia ni katibu,Sashisha
mafuwe ameeleza kuwa kati ya maeneo
ambayo yanaweza kupewa kipa umbele kwenye shughuli hiyo ya uelimishaji ni
pamoja na Mkoa huo kutokana na shughuli ambazo zimekuwa zikifanyika za uchimbaji.
Kwa upande
wao wadau ambao wanashirkiana na serikali kwenye mapambani ya kifua Dr,Kiva mvungi ambaye ni mganga mkuu wa mgodi
wa GGM ameelezea kuwa wao ni moja kati ya watu ambao wameendelea kupambana na
kifua kikuu kwa kuboresha maeneo ya kufanyia kazi hususani kwa wafanyakazi.
Bi,Ena
Lutenga ambaye anatokea shirika la umoja wa mataifa la wahamaji pia ameongeza wao wanashiriki katika kuweka
mazingira safi ya wakimbizi na kutokomeza ugonjwa huo kwenye maeneo ambayo ni
ya wakimbizi.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa Huo ambaye pia ni
Msaidizi wa katibu Tawala Mkoani Humo.Emmily Kasagara ,ameishukuru wizara ya
afya kupitia mpango wa kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu kuchagua Mkoa huo
katika utoaji wa elimu.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: