Baadhi ya wasanii ambao wameigiza kwenye filamu hiyo wakiwa nje ya ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Uzinduzi wa
Filamu ya Magwangala ambayo imechezwa na
wasanii wa Mkoani Geita pamoja na
viongozi wa Halmashauri ya Mji ulikuwa
ufanyike siku jana (Julai 27) umekwama kutokana na kuwepo kwa madai ya mgodi wa
dhahabu wa Geita(GGM) Kulalamika kuwa filamu hiyo inaonekana kuwa na mahudhui
ya uchochezi baina ya wananchi na mgodi
Mkoani humo.
Uzinduzi huo ulitarajia kufanywa na Naibu Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura Katika ukumbi wa Desire
Park .
Akizungumza juu ya hatua ya kukwama kwa uzinduzi huo Naibu waziri
Wambura,amesema
kuwa kilichotokea alipatiwa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kwamba kuna picha ambayo
sio nzuri na kwamba wao kama mgodi walilalamika juu ya picha hiyo na kwamba
wameangalia na kuona kuwa kuna maeneo ambayo yamerekodiwa sio mazuri na tatizo
ni mawasiliano baina ya Afisa utamaduni na Mkoa.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Humo ambaye pia ni moja kati ya
wachezaji wa Filamu Hiyo Bi,Rosemery
Michael ,amesema kuwa wao hawakuona mapungufu yoyote kwa maigizo ambayo wameigiza
kwenye filamu hiyo ni uhalisia wa maisha ambayo yapo ndani ya Mkoa usika.
Baadhi ya wasanii
na wananchi ambao wameudhuria siku ya jana kwenye uzinduzi wa Filamu
Hiyo,Sagari Mganga na Neema Philipo wamesema kuwa hata wao wameshindwa kujua ni
maswahibu gani ambayo yamejitokeza ambayo yamesababishwa filamu hiyo
kutokuzinduliwa.
Manase
Ndoroma ni meneja mwandamizi wa mgodi ambaye
anashughulika na maswala ya jamii, ndani ya Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) amefafanua
kuwa wao hawana ugomvi na sanaa wala na
wasanii ila kumetokea shida ambayo wametoa kwa jamii kwa makusudi na kwamba
mgodi huo una athari kwa jamii ambayo inauzunguka.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post A Comment: