Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika kwenye ukumbi wa hotel ya Alphendo Mjini Geita wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wa watu wanaishi na VVU (WAVIU). |
Kulia ni Bw.Shilambele Mussa na Bi.Magdalena Ngwada wakifanya maigizo ya namna ambavyo mhudumu anaweza kutoa huduma kwa mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi . |
MVIU mshauri Bi.Imelda Assey kutoka CTC ya hospitali ya wilaya ya Chato akisisitiza kuachana na dhana ya kuendelea kujinyanyapaa kwa watu wanaishi na VVU. |
Washiriki wakiwa kwenye vikundi wakijadili baadhi ya maswali. |
Mwezeshaji Bi.Amida Yindi akielekeza namna ambavyo MVIU mshauri anaweza kumhudumia mteja. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Shirika la lisilo la kiserikali la Ariel
Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na
mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya ya Geita Vijijini,Geita Mji ,Chato na Bukombe limewakutanisha
watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (WAVIU Washauri)kwa lengo la
kuwajengea uwezo wa kutoa elimu na kuwaunganisha wateja kutoka kwenye
jamii kwenda kwenye vituo vya tiba na matunzo(CTC).
Warsha hiyo
ambayo ilianza tarehe 29 January na inatarajia kumaliza tarehe 31january 2018 inafanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Alphendo
mjini Geita ikiwashirikisha washiriki 46
kutoka kwenye Halmashauri nne zilizopo Mkoani humo.
Afisa Miradi
Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe akizungumza wakati warsha hiyo amesisitiza
kwa WAVIU washauri kuunda vikundi kwenye CTC zao vya watu ambao wanaishi na virusi vya
Ukimwi ambavyo vitawasaidia kujiendeleza
kwenye shughuli za ujasiliamali pamoja na kushauriana katika matumizi ya dawa za kufubaza makali ya VVU.
Kambarangwe
ameeleza kuwa,kumeendelea kuwepo na tatizo kubwa la unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU hivyo kupitia warsha hii wamekuwa wakifanya jitihada za kutoa elimu kwenye jamii kwa kupitia WAVIU washauri ili kuondokana na dhana ya unyanyapaa.
Mmoja kati
ya watu ambao wanaishi na VVU kwa muda wa miaka 15, Bw. Eliya Malaki ambaye alipima VVU mwaka 2000
na kugundulika kuwa na maambukizi alisema "bado kuna watu katika jamii hawaamini kuwa wamepata maambukizi ya VVU matokeo
yake wanakimbilia kwa waganga wa jadi na wengine wamekuwa wakijinyanyapaa
wenyewe kwa kushindwa kufika kwenye vituo vya tiba na matuzo hili kupata ushauri na saa".
MVIU mshauri
wa Bi,Imelda Assey kutoka CTC ya hospitali ya wilaya ya Chato alisema "kupitia warsha ambayo
imefanywa na shirika la AGPAHI ni moja kati ya fursa ambayo itamsaidia
kuendelea kutoa elimu zaidi kwa watu ambao wanaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi,huku akisisitiza jamii ya watu ambao wanaishi na maambukizi kuachana na
dhana ya kujinyanyapa bali kuikubali hali hiyo na kuzingatia ushauri ambao
wanapewa na wataalamu wa afya ".
Mwezeshaji
katika warsha hiyo Bi,Amida Yindi ambaye
ni mratibu wa VVU na UKIMWI ngazi ya
jamii kwenye halmashauri ya wilaya ya Geita,amewasisitiza WAVIU washauri kujenga desturi
ya kufanya usafi kwenye vituo ambavyo wanafanyia kazi pamoja na kuangalia kadi
za wateja kama zimekusanywa na kuwekwa mahali ambapo ni sahihi.
Post A Comment: