Baadhi ya eneo ambalo linalalamikiwa na Bw,Sizya Mashirungu kuvamiwa na kujengwa shule na serikali kinyume na makubaliano kati yake halmashauri ya Mji wa Geita. |
Mwenyekiti wa mtaa Shinde Bw Makoye Mumilambo akizungumza juu ya malalamiko ambayo yametolewa na Bw,Sizya Mashirungu juu ya kutaka kutahifishwa eneo la familia na serikali ya mtaa huo. |
Eneo linalolalamikiwa likiwa tayari limeshaanza kuchimbwa Msingi kwaajili ya ujenzi wa shule ya Msingi ya Shinde. |
Na,Joel Maduka,Geita.
Familia ya
Bw Mlelemi Mashirungu inayoishi mtaa wa Mkolani Kata ya Nyankumbu wilayani
Geita imeilalamikia serikali kwa kuanzisha ujenzi wa shule ya msingi Shinde
kwenye shamba la ukoo huo lenye ukubwa wa ekari 20 bila makubaliano na serikali
ya Halmashauri ya mji wa Geita .
Msimamizi wa
eneo hilo Bw Sizya Mashirungu amesema
eneo la ujenzi wa shule hiyo lilitengwa na serikali ya kijiji kabla ya
kubadilishwa na kuwa mitaa lakini ameshangazwa na kitendo cha serikali
kuanzisha ujenzi katika eneo lake bila makubaliano.
Bw Mashirungu
alisema eneo hilo limeanza kumilikiwa na
ukoo tangu mwaka 1991 baada ya Baba yao mzazi kufariki na kwamba limekuwa
likitumika katika shughuli za kilimo.
“Anayezungumza
kuwa hii ni hifadhi akuna ofisi yoyote ambayo ilishawai kufika kuweka pingamizi
juu ya eneo hili na mshangaa mwenyekiti ambaye anangangania kuwa eneo hili ni
la hifadhi yani huu ni utapeli kabisa na mimi sitakubaliana na maamuzi ambayo
yanataka kuchukuliwa na serikali juu ya matumizi ya eneo hili”Alisema Mlelemi.
Aidha
kutokana na malalamiko kumuelekea Mwenyekiti wa mtaa huo Bw Makoye Mumilambo
kutaka kuhujumu eneo la ukoo huo, Kwa upande wake amesema eneo hilo lipo ndani
ya hifadhi ya halmashauri ya mji wa Geita na kwamba watu wamekuwa wakimiliki
maeneo hayo kinyume na utaratibu tangu mwaka 1978 na kwamba hata yeye ni
mvamizi kutokana na miti iliyokuwepo kukatwa hivyo serikali imeamua kubadili
matumizi ya eneo hilo.
Diwani wa
kata hiyo Bw Machael Kapaya alisema madai ya Bw Masirungu sio ya kweli kwa kuwa
miradi inayoanzishwa michakato huanzia kwenye ngazi ya chini ambayo ni wananchi
ambao wanapendekeza mahitaji yao na kwambe yeye
ni moja kati ya viongozi wa mitaa na anajua utaratibu.
“Huyu ni
kiongozi kabisa wa mtaa na anajua taratibu zote ambazo zinafanyika kuibua
miradi kwenye mitaa na wakati tunapendekeza eneo hilo alikuwepo kwenye kikao
cha kamati ya maendeleo ya kata na tulikwisha mwambia kama anamadai alete
vielelezo ambavyo vinathibitisha kuwa ni eneo lake lakini hadi sasa ajaleta na
tukimwambia aje kwa mkurugenzi anachenga chenga”Alisema Kapaya.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modesti Apolinary alisema eneo
linalotumika katika ujenzi wa shule ni eneo la hifadhi na kwamba hakuna mtu
anayeruhusiwa kumiliki eneo lililo ndani ya hifadhi ya serikali.
Post A Comment: