Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mkoani Geita, ,Bw Charles Kazungu Akitoa msaada kwa Bi, Teddy Saidi wakati wa zoezi la kutoa misaada katika kuadhimisha miaka 41 ya chama cha mapinduzi Wilayani Geita. |
Baadhi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi wakiwa wameambatana na Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mkoani Geita, ,Bw Charles Kazungu wakitoa msaada kwa mtoto Zuberi Juma. |
Mjumbe wa Baraza kuu Taifa Mkoani Geita, ,Bw Charles Kazungu akitoa msaada kwa Bw,Fredy Magunga. |
Katibu wa chama cha mapinduzi(CCM)Julius Peter akitoa pole kwa mgojwa ambaye alikuwa kwenye wodi ya wakinamama Hospitali ya Rufaa ya Mkoani Geita. |
Consolata Evarist.Geita
|
Chama Cha
Mapinduzi(CCM) Wilayani Geita kimeadhimisha miaka Arobaini na moja (41)
tangu kuzaliwa kwa kuwatembea wagonjwa na
kutoa misaada mbali mbali kwenye hospatali ya Rufaa ya mkoani humo.
Zoezi hilo limeendeshwa
na uongozi wa chama na baadhi ya wanachama
wakiambatana na Mjumbe wa Baraza
kuu Taifa ambaye alikuwa ni mgeni Rasmi ,Bw
Charles Kazungu alisema maamuzi
ya kutembelea hospitali ya mkoa ni kutaka kujua namna ambavyo ilani ya chama
hicho inavyotekelezwa kwenye sekta ya
afya.
Aidha ametoa wito kwa
watumishi wa Sekta hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia taratibu na
sheria ambazo zimewekwa na nchi.
“Natoa wito kwa
watumishi ambao wanatabiaya kutokutoa huduma vizuri kwa wagonjwa kuachana na
tabia hiyo rai yangu waweze kutimiza
adhima na kazi zao utawala wa chama cha mapinduzi hususani awamu ya tano
unataka wafanye kazi kwa mujibu na sheria nasi vinginevyo”,alisema Kazungu
Kazungu alisema katika
kuhakikisha serikali inajali wananchi wake imeonelea ni vyema maadhimisho kwa ngazi ya wilaya
wakayafanyia hospalini na kutoa msaada
wa kuwasaidia watu ambao wanauwitaji maalumu kama wagonjwa.
Pia amewataka wananchi kufika katika vituo vya afya kwani
vimeboreshwa kwa kiasi kikubwa na vina hudumia kwa umakini mkubwa hivyo
wasipendelee kukaa na magonjwa nyumbani wanaweza kusababisha vifo na matatizo
makubwa ambayo yange weza kuzuilika.
kwa upande wake katibu
wa umoja wa wazazi Wilaya ya Geita,Happynes James ameiasa jamii pindi inapopata matatizo ya
kiafya ni vyema wakafika kwenye vituo vya afya ili kujua ni matatizo gani ambayo
yanawasumbua na kuachana na dhana ya kukimbilia wa waganga wa kienyeji
Baadhi ya wagonjwa
akiwemo Teddy Mathayo na Juma Mabeyo wameishukuru serikali pamoja na chama cha
mapinduzi (CCM) kwa msaada ambao wameutoa kwa moyo walio uonesha wakuonesha
kujali na kuwafariji kwa kiasi kile walicho balikiwa na kwamba wamefarijika sana kwa tukio hilo .
Post A Comment: