Mkuu wa mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita juu ya kuendelea kuwatumia mafundi wa ngazi za mitaa (Local fundi) kwenye miradi ya jamii. |
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita ,Elisha Lupuga akizungumza na madiwani wakati wa kikao cha kawaida cha robo ya pili cha baraza hilo. |
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha kawaida cha robo ya pili cha baraza. |
Na,Maduka Joel ,Geita
Madiwani wa
Halmashauri ya wilaya ya Geita wametakiwa kubuni mbinu zitakazoleta Maendeleo
kwenye Kata zao pamoja na kushughulikia utatuzi wa kero za wananchi kwenye
maeneo yao.
Akizungumza
wakati wa kikao cha kawaida cha robo ya pili cha baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw Elisha Lupuga amewataka Madiwani hao
kuwatumikia wananchi kikamilifu na kuachana na mambo yanayoweza kuzorotesha
maendeleo.
“kipindi
hiki ni cha kufanya kazi na kuwatumikia wananchi Utakiwi kuwa diwani wa
kulalamika kwani ukuchaguliwa na wananchi hili uwe kiongozi wa ambaye unakuwa
na malalamiko bila ya kutafuta njia ambazo zinaweza kusaidia kutatua changamoto
za wananchi ambao unawaongoza natambua Rais wetu kwasasa anasisitiza tufanye
kazi za kuwatumikia wananchi wetu”Alisisitiza Lupuga.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi aliwataka madiwani
na wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Geita kufanya kazi kwa ushirikiano
kuhakikisha wilaya hiyo inapiga hatua na kuchochea maendeleo ya wananchi.
Pia
amesisitiza suala la kutumia mafundi wa ngazi za mitaa katika kukamilisha
ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule na afya ili kupunguza gharama za
wakandarasi ambao hutoza fedha nyingi.
Mhandisi
Luhumbi pia amewakumbusha madiwani kuhoji miradi yote kwenye kata zao na
Halmashauri kwa ujumla ambayo inafadhiliwa na mgodi wa dhahabu wa Geita, GGM
kwa madai kuwa baadhi ya miradi imekua na gharama kubwa kuliko uhalisia wake.
Post A Comment: