Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondary ya Mwatulole,Bi Roselyine Mdariki akishukuru kuwenza kupatiwa msaada huo kwenye shule hiyo ambao utasaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa. |
Mzee Devid Ng’ombeyapi akielezea namna ambavyo aliguswa na kuamua kuchangia kwenye sekta ya Elimu. |
Baadhi ya vyumba vya madarasa kwenye shule ya Sekondary Mwatulole. |
Mzee Devid Ng’ombeyapi akibidhi seruji kwa Diwani wa kata ya Buhala hala( kushoto) Musa Kabese Pamoja na kwa mkuu wa shule ya Sekondary ya Mwatulole Bi,Roselyine Mdariki. |
Wakazi wa
Halmashauri ya mji wa Geita wameombwa kuendelea kuunga Mkono jitihada za kutoa
michango mbalimbali itakayosaidia kuboresha miundombinu ya Elimu.
Wito huo
umetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mhandisi Modest Apolinary wakati
akipokea mifuko 10 ya seruji na tripu mbili za mchanga kwenye shule ya
sekondari ya Mwatulole kutoka kwa mwananchi aliyejitolea kwa lengo la kusaidia
ujenzi wa mabweni shuleni hapo.
Alisema
suala la kutoa michango alijakataliwa jambo ambalo lilizuiliwa ni walimu kuendelea
kujihusisha na kupokea michango na wengine walikuwa wakiwarudisha wanafunzi
sababu tu ya kukosa michango jambo ambalo sio sahihi na kwamba kwa mtu ambaye anaguswa ni vyema
wakawasiliana na ofisi ya mkurugenzi mtendaji.
Aidha kwa
upande wake Mkuu wa shule ya sekondari mwatulole Bi,Roselyine Mdariki mbali na kushukuru kwa
msaada huo ameelezea changamoto ambayo wanaipata kwa sasa shuleni hapo ni
upungufu wa madarasa kwani kwa mwaka huu
wamepokea wanafunzi wengi zaidi wa kidato cha kwanza ukilinganisha na miaka
iliyopita.
“Shule yetu
imekuwa na changamoto ya vyumba vya madarasa kutokana na ongezeko la wanafunzi
kwa mwaka huu na kutokana na ongezeko hilo mkurugenzi wetu wa halmashauri
ameamua kutuunga mkono kwa kutupatia mifuko ya seruji mia moja tunaamini
itasaidia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapa”Alisema
Mdariki.
Hata hivyo
diwani wa kata ya Buhala hala,Musa Kabese ,alisema changamoto kwenye kata yake
ni ni upungufu mkubwa wa madarasa ambapo vinaitaji vyumba kumi na moja hili kukidhi mahitaji kwa shule mbili za sekondari mwatulole pamoja na kalangalala .
Kwa upande
wake mwananchi ambaye ametoa msaada huo,Devid Ng’ombeyapi alisema
kilichopelekea kutoa ni kutokana na kuguswa na namna ambavyo wanafunzi wamekuwa
wakipata shida ya upungufu wa vyumba vya
madarasa shuleni hapo.
Post A Comment: