Na,Consolata
Evarist,Geita
Mbunge wa
jimbo la Geita mjini Constantine Kanyasu, amepinga tamko la mkurugenzi mtendaji
wa halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modest
Apolinary alilolitoa hivi karibuni akiwataka wasafirishaji wa
abiria kwa kutumia Baiskeli maarufu kwa jina la Daladala kusitisha shughuli
hizo mjini Geita kwa madai kuwa wamekuwa chanzo cha ajali mjini humo.
Bw Kanyasu
akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati akisikiliza na kujibu kero za
wananchi wa mtaa wa Barabara ya Msalala Kata ya Kalangalala alisema kuwa muda
wa kuwazuia waendesha baiskeli kutoa huduma hiyo haujafika bali waendelee
kufanya kazi bila kubughudhiwa .
Alisema kuwa
aliyetoa tamko la kuwazuia waendesha Baiskeli hao kwa madai kuwa wanasababisha
ajali mjini hakufanya utafiti na kwamba
hakuna kikao cha Baraza la madiwani kilichoketi na kukubaliana kuwa waendesha
baiskeli hao maarufu Daladala wasitishe kutoa huduma hiyo mjini hivyo
wataendelea kutoa huduma ya kubeba abiria kama kawaida.
Bw Kanyasu
alisema kuwa mji wa Geita unakuwa lakini
yeye binafisi amefanikiwa kufika
China licha ya kupiga hatua kubwa kimaendeleo pamoja na teknolojia wananchi wa
Taifa hilo bado kwenye barabara zao wanaendesha baiskeli hivyo bajaji na
Pikpiki maarufu kama bodaboda pamoja na daladala waendele kufanya kazi kwa kufuata sheria za barabarani
kwa kuwa wote wana haki ya kutafuta riziki kwa kutumia kazi zao.
''Waendesha daladala za baikeli, Bajaji na
waendesha Pikipiki wote wana haki ya kufanya kazi, aliyetoa tamko la kuzuia
baiskeli hakufanya utafiti kwanza na hakuna kikao chochote walichokaa madiwani
wakakubalina, hivyo muda ukifika watajiondoa wenyewe ", alisema Kanyasu .
Aidha katibu
wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi, UVCCM wilayani Geita Bw Rajab
Ally Rajab akitoa salaam za chama hicho
kwenye mkutano huo alipinga hatua ya mkurugenzi huyo na kusema kuwa serikali
haiwezi kuwazuia waendesha Baiskeli hao kutoa huduma hiyo mjini bila
kuwaandalia mazingira ya eneo la kutolea huduma hiyo na kwamba chama hicho
hakiko tayari kuona vijana wanahangaika .
"Wanaofanya
kazi ya kuendesha daladala za baiskeli wengi ni vijana na ni wapiga kura wa chama change, Chama hakiwezi kukubali watimuliwe mjini watafanyia kazi zao
wapi bila kuwaandalia mazingira? Mkurugenzi hakukishirikisha chama tulishituka
baada ya kusikia matangazo", alisema katibu Ally Rajabu.
Hivi
karibuni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita aliwatangazia
waendesha daladala za baiskeli kusitisha kutoa huduma ya kubeba abiria mjini na
badali yake wafanye shughuli zao kwenye maeneo ambayo walikuwa wamepangiwa
yakiwemo ya Nyankumbu na Mwatulole pembezoni mwa mji
kwa madai kuwa wamekuwa chanzo cha ajali za barabarani mjini hali
iliyosababisha kuibua maandamano makubwa
ya waendesha daladala hadi katika ofisi za mbunge wa jimbo la Geita
mjini .
Post A Comment: