|
Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Geita,Rose Michael (ROSE BONANZA)Akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashinda ya wasanii wa maigizo na nyimbo mbele ya mgeni rasimi kwenye ukumbi wa halmashauri ya mji wa Geita. |
|
Meza kuu ikiongozwa na mgeni rasimi ambaye ni afsa maendeleo wa halmashauri ya Mji ndugu,Maiga Majagi aliyevaa shati ya dirafti katika katika. |
|
Msanii wa nyimbo za asili katoka kata ya Bukoli akiburudisha wakati wa mashindano hayo |
|
Meza kuu ikifatilia kwa makini kile ambacho kilikuwa kinaendelea |
|
Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Geita,Rose Michael (ROSE BONANZA) akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa. |
|
Moja kati ya majaji katika mashindano hayo,Bi Anithar Kagemulo akijitambulisha wakati wa mashindano hayo. |
|
Kikundim cha uwimbaji kutoka wilayani Chato cha Mwagazege kikiimba katika mashindano hayo. |
|
Mgeni rasimi ambaye ni afsa maendeleo ya jamii Ndugu Maiga Majagi akizungumza na wasanii huku akiwaasa kuendeleo kuwa na umoja na kushikamana ili kuendeleza sanaa katika Mkoa wa Geita. |
|
Mgeni rasimi ambaye ni afsa maendeleo ya jamii Ndugu Maiga Majagi ,akiendelea na hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mashindano. |
|
Meza kuu ikimsikiliza mgeni rasimi wakati wa hotuba yake |
|
Majaji wakifatilia mashindano |
GEITA:Chama cha wasanii Mkoani Geita,kimeiomba
serikali Mkoani humo kuendelea kutoa ushirikiano katika Nyanja hiyo muhimu
ikiwa ni pamoja na kusapoti kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na wasanii.
Kauli hiyo imesemwa na mwenyekiti wa chama hicho
Mkoani Humo Rose Michael wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuwasaka wasanii
wenye vipaji vya kuimba kuigiza na kuchekesha yaliyokuwa yanafanyika katika
ukumbi wa halmashauri ya Mji wa Geita.
Rose alisema kuwa Tasnia ya sanaa bado inachangamoto
nyingi ikiwa ni pamojan na kushindwa kutambulika na kushikwa mkono kwenye serikali kutokana na kwamba baadhi viongozi wa kiserikali wanaona swala la
wasanii limekaa kiunu jambo ambalo si kweli kwani kazi ya sanaa ni sawa na shughuli zingine
katika jamii.
“Sisi wasanii bado tunachangamoto kubwa sana katika
serikali ingawa kwa sasa kuna wizara inayotutambua lakini bado kuna ugumu
mwingi tu tukiangali kwenye serikali kuna viongozi ambao wanaona kuwa hatuna
mchango wowote lakini sio kweli sisi tunauwezo wa kufikisha ujumbe kwa jamii na
ikatuelewa zaidi kuliko vile ambavyo serikali imeendelea kutuchukulia”alisema
Rose.
Kwa upande wake mwenyekiti wa waigizaji Mkoa wa
Mwanza,Ramadhani Masululi,amesema kuwa
jambo ambalo limekuwa likisababisha sanaa au wasanii kuonekana ni wahuni ni
kutokana na baadhi ya wasanii kuonekana kutokujieshimu na wengine kuingia
kwenye sanaa bila ya kuwa na maono au mtazamo chanya katika sanaa.
“Sanaa sio uhuni kwanini wanasema uhuni waigizaji wengine wameingia ni mamluki unakuta mwingine anaingia kwenye sanaa
ni mlevi mvuta bangi na mwingine ni Malaya na hii ya wezekana kwasababu
nikutokana na vigezo kutokuwa vigumu lakini sisi kama chama cha wasanii hatuwezi kukubaliana na swala
hili tutaakikisha wale wenyetabia za ajabu wanatupisha ili tuwe na wasanii
ambao wananidhamu”alisema Ramadhani
Akimwakilisha Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa
Geita ambaye ndiye alikuwa mgeni rasimi kwenye uzinduzi huo,afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri hiyo,Maiga Majagi,amewaasa
wasanii kutumia umoja wao kuleta
mabadiliko kwa wanageita kwa kufanya kazi na kukitumia chama chao kwa kuwa
tetea zaidi na kupata taarifa mbali
mbali za soko la kazi zao na pia amewataka
kupanga mikakati ya kushirikiana
na wadau wote na kwamba jambo likiongelewa na wote linakuwa
na nguvu kuliko kuzungumziwa na mtu mmoja.
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE
Post A Comment: