Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza wakati alipofungua kikao cha wizara hiyo na wamiliki wa vyombo vya habari ili kujadili na kuweka mkakati wa pamoja katika kuhamasisha watanzania kujiandaa na kuingia katika utekelezaji sera ya serikali ya ujenzi wa viwanda ili Tanzania iweze kufikia lengo la kuwa nchi ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2020 kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Magazeti ya serikali (TSN) Jim Yonaz na katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel, Mkutano huo umefanyika kwenye ofisi za wizara hiyo uwanja wa Taifa.
Mh. Nape Nnauye Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza kumkaribisha Waziri huyo ili kuzungumza na wadau wa vyombo vya habari katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi za wizara hiyo Uwanja wa Taifa, kushoto ni Dk Jim Yonaz Mkurugenzi wa TSN.
Mh. Nape Nnauye Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelelzo Dk. Hassan Abbas wakati alipokuwa akitoa mada kwa wadau wa vyombo vya habari kuhusu namna wadau hao wanavyoweza kushirikiana na serikali katika kuhamasisha uwekezaji na ujenzi wa viwanda nchini.
Mhariri Mtendaji wa Gaseti la Jambo Leo Bw. Theophil Makunga akichangia hoja katika mkutano huo.
Mhariri Mtendaji wa ITV Bw. Steven Chuwa akichangia hoja katika mkutano huo
Baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari wakiwa katika mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakifuatilia hoja mbalimbali katika mkutano huo.
Mh. Nape Nnauye Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo leo.
Post A Comment: