HALMASHAURI ZIPELEKE MAAFISA UGANI VIJIJINI KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA.
Halmashauri za Wilaya katika maeneo ambayo yanalimwa zao la Pamba hapa nchini, zimetakiwa kuwapeleka Maafisa Ugani katika Vijiji vyao kwa ajili ya kutoa Elimu juu ya Ulimwaji wa zao hilo kwa lengo kurudisha hadhi yake kama ilivyokuwa katika mika ya nyuma.
Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi wa zao la Pamba hapa nchini James Shimbe aliyasdeha hayo katika ziara yake ya siku moja Wilayani hapa kwa ajili ya kukagua Viwanda vya uchambuaji wa zao la Pamba na kusisitiza juu ya upelekwaji wa mbugu bora kwa Wakulima katika msimu ujao wa zao Pamba.
Shimbe alisema kama Halmashauri za Wilaya zitaweza kupeleka maafisa Ugani katika maeneo ambayo ni marufu kwa kilimo cha zao hilo basi kunaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa Wakulima katika kulima kilimo cha Pamba kilicho bora na chenye tija na kupelekea kupata mavuno mengi.
Alisema kuwa katika msimu uliopita wa Pamba Wakulima walipata Pamba iliyo bora kutokan na kupata maelekezo kutoka kwa Wataalamu wa zao hilo ikiwa ni pamoja na Bodi ya Pamba kutoa Semina kwa Wahasibu juu ya ununuzi wa Pamba safi ambayo itakuwa haikuwekewa maji wala michanga.
“Asilimia 99 ya Pamba iliyolimwa katika msimu uliopita katika baadhi ya sehemu hapa nchini ilikuwa ni bora na ni safi na hali hii kama itaendelea hivi basi hata katika soko la Dunia bei ya Pamba yetu ya Tanzania inaweza kupanda bei mara dufu tofauti na ilivyokuwa hapa awali”, Alisema Mkurugenzi huyo James Shimbe kutoka Bodi ya Pamba nchini.
Aliendelea kusema kuwa hali hiyo ilitokana na udhibiti wa ubora wa Pamba wakati wa ununuzi na kuongeza kuwa katika msimu huu ujao tayari Viwatilifu vipo karibu kuwafikia Wakulima kabla ya mwezi wazi tisa ili kuhakikisha kuwa wakulima harudishwi nyuma katika kilimo cxha Pamba.
Kwa upande wake mmoja wa Wakulima wa zao la Pamba kutoka katika kata ya Ukune Deogratius Makaranga alisema kuwa kupatikana na Pamba iliyo bora katika usimu ulipita ulichangiwa na kuwajibishwa kwa Wahasibu ambao walikwenda kinyume na taratibu zilozowekwa na Bodi ya Pamba.
Makaranga pia aliishauri Bodi ya Pamba hapa nchini kuhakikisha kuwa madawa yanafika kwa wakati katika sehemu husika ikiwa ni sambamba na Wamiliki wa Viwanda vya kuchambulia zao hilo kutochelewesha Mbegu kuwafikia maktika maeneo yao ya ulimwaji wa zao hilo.
Alisema kuwa Bodi ya Pamba kupitia kitengo cha udhibiti wa Mbegu (TOSKI) ihakikishe kuwa inazikagua mbegu hizo kama ni bora kabla ya kusambazwa kwa Wakulima hali ambayo inaweza kuchangia kuweza kugundua Mbegu ambazo zitakuwa ni bora na zile ambazo zitakuwa sio bora na kupunguza changamoto iliyopo ya mbegu kutoota.
Akizungumzia kuhusu suala la uchafuzi wa Pamba Makaranga alisema kuwa anayechafua Pamba sio Mkulima bali ni Wahasibu na kuongeza kuwa Serikali kwa sasa haina budi kushirikiana na Makampuni ya ununuzi wa Pamba hali ambayo itapelekea kupatikana kwa Pamba safi na yenye tija kwa nchi kila mwaka.
Post A Comment: