Na COSTANTINE MATHIAS, BARIADI
WANANCHI wa Kata ya Gamboshi wilayani Bariadi mkoani Simiyu
wamemwomba waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako kufika
katika kijiji hicho ili kutatua changamoto za kielimu zinazolikabili kijiji
hicho. na kulifanya kuwa nyuma kimaendeleo.
Mbali na Waziri huyo, Viongozi wengine ambao wamekuwa
wakiogopa kufika eneo hilo kutokana na historia yake kuwa ni kijiji cha wachawi
wameombwa kufika na kutatua changamoto hizo ili kuifuta dhana iliyokuwa
imejengeka kuwa ni ki jiji cha wachawi.
Akiwasilisha maoni hayo ya wananchi kwenye misa ya kipaimara
iliyoadhimishwa kijijini hapo, Diwani wa kata hiyo Bahame Kaliwa amemtaka
waziri huyo kufika ili kujionea changamoto za kielimu hasa wingi wa wanafunzi
madarasani na pia ajionee miundombinu
duni ambayo hawawezi kuimaliza kwa haraka.
‘’hii dhana ya
ushirikina iliyokuwa imejengeka haiwezi kuondolewa bila elimu…hivyo tunamwomba
waziri wa elimu tunamwomba afike hapa aje aone watoto walivyowengi, na aone miundombinu
ilivyoduni ambayo haiwezi kuondolewa kwa uharaka, hasa neon lililojengeka la
ushirikina’’ alisema Kaliwa.
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu
Liberatus Sangu amewataka viongozi wa serikali kuyafikia maeneo ambayo yalikuwa
yamesahaulika ikiwemo Gamgoshi, na kuyapelekea miundombinu na kuwafungua watu
hao ili waweze kubadilika kifikra, kimaono na kimtazamo.’
Sangu aliongeza kuwa ikiwezekana wanafunzi wote waliohitimu elimu
ya msingi kijijini hapo wawe wamefaulu au hawajafaulu waende sekondari ili
baada ya kuhitimu waweze kuibadilisha jamii ya eneo hilo, na kuwafungua wapate
elimu.
‘’viongozi wa ngazi za serikali waje kuyafikia maeneo hayo…wanafunzi
wote waliohitimu darasa la saba waende wote sekondari hata kama hawajafaulu ili
kuibadili jamii yao iweze kuondokana na ukatili wa mauaji ya watu wenye ulemavu
wa ngozi kwa sababu wote wamezaliwa na kuumbwa kwa sura na mfano wa mungu’’
alisema Sangu.
Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria Maadhimisho ya misa
hiyo takatifu ya kipaimara walisema kuwa eneo hilo kwa sasa ni tulivu tofauti
na inavyoaminika kwa sababu ni sawa na maeneno mengine ya nchi na watu
wanaoishi huku ni wa kawaida sana, alisema Danieli Mvungi kutoka Morogoro
aliyekuwa amehudhuria misa hiyo.
Padri wa parokia ya Ngulyati John Nkinga alisema kuwa hadi
sasa kuna mabadiliko makubwa kutokana na watu wa eneo hilo wameanza kubadilika kiimani
kwa kumcha mungu, ambapo jumla ya waimarishwa 200 walipewa kipaimara katika
kanisa la Mtakatifu Petro Gamboshi.
|
Post A Comment: