Baadhi ya vikundi vya wajasiriamali wakifuatilia Semina ambayo ilikuwa inafanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Mji wa Geita. |
Kikundi cha wasaniii ambacho kinajihusisha na shughuli za ujasiriamali kikifuatilia semina. |
Chama cha wafanyabiashara, wenye viwanda na
wakulima, TCCIA Mkoani Geita kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Nchini (TRA)
imewakutanisha wafanyabiashara wadogo na wakubwa kwa lengo la kuwapatia
elimu ambayo itawasaidia kulipa kodi.
Akizungumza na wafanyabiashara hao ambao walikuwa
wamejitokeza kwenye ukumbi wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mgeni Rasmi ambaye ni
Mkuu wa Wilaya ya Geite ,Mwl Herman
Kapufi ,amesema wajasiriamali wanatakiwa kusajiliwa na kujua elimu ya mlipa
kodi ambayo itawasaidia kujulikana na
kutambulika serikalini.
Akizungumza na MADUKAONLINE Meneja wa TRA Mkoani Geita,James Jilala
,amesema kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria za nchi wafanyabiashara ambao wanakuwa sio rasmi wanatakiwa kuwa
kwenye vikundi maalum ambavyo vitatambuliwa na kupatiwa elimu ambayo
itawasaidia kuwa walipa kodi wazuri.
Katibu wa
TCCIA Mkoani Humo,Mariam Mkaka ameelezea kukosekana elimu ya ujasiriamali ni
chanzo ambacho kimekuwa kikisababisha vikundi vingi kutokusimama na kujikuta
vinaanguka.
Baadhi ya
wafanyabiashara wadogo ambao wameshiriki
katika semina hiyo,Rose Michael ,Jackson Mlenga na Winfrida Marius wameeleza
kuwa semina hiyo itawasaidia kupata Elimu ya ulipaji Kodi.
Post A Comment: