Pikipiki zilizotolewa zikiwa zimepakiwa |
Katibu wa CCM kata ya buziku,Bahati Mayengera. |
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC),Deodedisi Katware |
Mnec akifafanua jambo na wajumbe. |
Wajumbe wakifatilia kwa makini maagizo ya Mnec. |
Bw,Katware akikabidhi pikipiki kwa viongozi. |
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama akijaribia kuwasha moja kati ya pikipiki. |
Jumla ya
pikipiki 31 zenye thamani ya milioni 806,000,000 zimetolewa kwa makatibu wa Chama cha
mapinduzi (CCM)ngazi ya vitongoji ,vijiji na kata wilayani chato mkoani geita
lengo likiwa ni kuakikisha wanaimalisha chama kwa kuraisisha utendaji wa kazi.
Hayo yamesemwa
na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC),Deodedisi Katware,wakati wa zoezi
la ugawaji wa usafiri huo,ambapo alisema kuwa kutokana na kwamba kwa sasa kumekuwepo na
ushindani wa kisiasa wanaamini kuwa kuwapatia pikipiki hizo zitasaidia kufanya kazi
zao kwa wepesi na kuwatumikia wananchi kama ambavyo walihaidi kuwatumikia
kwenye uchaguzi wa mwaka jana.
”Lengo kubwa
la kutoa usafiri kwa viongozi wa chama ngazi ya kata kwa maana makatibu kwanza
ni kuimalisha na kukiendeleza chama na tunatamani viongozi hawa wa ngazi ya
kata watekeleze majukumu yao kama inavyotakiwa”alisema katware.
Akizungumza kwa
niaba ya makatibu ambao wamepatiwa pikipiki hizo,katibu wa ccm kata ya Buziku,Bahati
Mayengera,alisema kuwa kipindi cha nyuma wakati hawajapatiwa usafiri huo
walikuwa na changamoto kubwa ya kutembea umbali wa kilomita nyingi kwaajili ya
kwenda kutoa huduma kwa wananchama ambao wana maitaji.
“Kipindi cha
nyuma wakati hatujapewa usafiri huu tulikuwa na shida sana hasa wakati wa
kapeni na shughuli zingine za chama lakini kwa sasa kwa kuwa tumepatiwa usafiri
huu tunaamini utatusaidia kuondoa usumbufu wa kutembea kwa baskeli.”Alisema Mayengera
Pamoja na
kumpongeza kiongozi wa NEC,viongozi hao wamewaomba viongozi waliopo ngazi ya Taifa
kuwakumbuka wale ambao wapo chini kwa kuiga mfano huo na kuwa na moyo wa kutoa kama
ambavyo amefanya bw katware kwani ngazi ya kata na vijiji wamekuwa
wakisahaulika sana hali ambayo inapelekea kudhorotesha utendaji kazi wa chama.
Imeandaliwa
na Madukaonline.
Post A Comment: