Wanachuo wakiwawakiwa katika makundi makundi wakisubili kujua mwafaka wa pesa zao. |
Wakifatilia kwa makini kikao na mkuu wa wilaya. |
Mkuu wa chuo ambae anatuhumiwa kula pesa za wanafunzi,mwalimu Sindano Masanja. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi,akitoa maagizo juu ya malipo ya wanachuo wa rich rice |
Nyaraka za siri za serikali zilizokutwa kwenye ofisi ya mkuu wa chuo. |
mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi,Tungalaza George,akitoa ufafanuzi juu ya uchunguzi waliofanya. |
Kaimu mkurugenzi wa chuo hicho Bahati charles |
Mhasibu na mtaaluma wakiwa chini ya ulinzi. |
Wanachuo wakiteta jambo na Mkuu wa wilaya. |
Walio jaribu kutorosha fedha wakiwa wamekamatwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. |
Wanafunzi wakisubilia malipo yao. |
GEITA:Kaimu
mkuu wa mkoa wa geita ambaye ni mkuu wa
wilaya ya geita hermani kapufi ameamuru kuwekwa ndani kwa aliyekuwa mkuu wa chuo cha ualimu
geita cha rich rise,mhasibu na mkurugenzi wa chuo hicho baada ya kushindwa
kurejesha ada za wananchuo wapatao 300
wa mwaka wa kwanza kiasi cha milioni 230 .
Hatu hiyo ya
kutaka kurejeshewa fedha zao imejiri baada
ya uongozi wa chuo hicho kuendelea kudai kuwa wanafunzi wa mwaka wa
kwanza kozi ya ualimu wa chakechea yani
ecde ambayo kwa sasa haitambuliwi
na baraza la mitihani la taifa necta kutokana na kufutwa .
Akitoa
maelezo kwa kaimu mkuu wa mkoa,kaimu mkurugenzi wa chuo hicho Bahati
charles,alimwomba mkuu wa mkoa kuwaomba
wanafunzi wapokee kiasi cha sh,milioni115
huku wakiendelea kutafuta pesa
zingine za kutoa fidia kwa wanafunzi hao.
“Zoezi la
kwanza ndungu mkuu wa mkoa uliagiza tuwapatie vyeti zoezi hilo tumeshakamilisha
kwa asilimia tisini zoezi la pili ni kuhusu pesa tatizo kubwa lililokuwepo hapa
ni kuanzisha kozi ya ECDE ambayo hipo kinyume na taratibu kutokana na kuagiza
vijana wote wapewe pesa zao uwangozi wa chuo umeandaa nusu ya pesa ambayo
watalipwa vijana na pesa itakayobakia watalipwa kwa awamu nyingine”alisema
Charles
Hata hivyo
kwa upande wake, mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi,Tungalaza George,alisema kuwa
wamefanya ukaguzi katika ofisi ya mkuu wa chuo hicho na kubaini kuwa kuna nyara
za siri za serikali zimetumika zisivyo kwani kunamitihani ya Taifa ambayo
inatakiwa kuwa Necta imekutwa ikiwa ndani ya ofisi.
Baada ya
maelezo hayo mkuu wa wilaya ambae pia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Geita,Herman Kapufi,alitoa
maagizo ya kukamatwa kwa mkurugenzi na mhasibu na mkuu wa chuo aliyekuwapo
chuoni hapo kipindi cha nyuma,Sindano Masanja.
“Na
kwasababu tumefikia katika hatua hii na
taarifa niliyohipata ni kwamba kuna milioni 115 haya kama ni milioni 115 maelekezo yangu ni kama ifatavyo mmiriki wa
chuo,mhasibu,mwalimu wa taaluma Ruben Kubwa ,meneja wa shule naomba mkae pale chini
ya ulinzi paka zipatikane hizo fedha.”alisema Kapufi.
Baadhi ya
wanachuo chuoni hapo wamepongeza uwamuzi huo wa kaimu mkuu wa mkoa wakiamini
kuwa watapatiwa haki zao ambazo walikuwa wakidai,lakini pia wamelalamika kwa
kusoma kozi hewa ambayo imeshafutwa muda mrefu.
Mkuu huyo
amesema wanachuo hao wasiondoke chuoni hapo mpaka watakapopewa fedha zao zote na
mala baada ya kulipa fedha hizo viongozi watachukuliwa hatua
kwa makosa madogo ambayo yamejitokeza chuoni hapo.
Lakini katika
hali isiyo ya kawaida baadhi ya watumishi chuoni hapo walionesha kukiuka agizo
la DC na kutaka kutorosha fedha ambazo zilitakiwa kugawiwa wanafunzi lakini
hata hivyo awakufanikishwa kwani kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ilikuwa
macho na mwisho wa siku waliwekwa chini ya ulinzi kwa kosa la kujaribu kutaka
kutorosha fedha hizo.
Imeandaliwa
na Joel Maduka
Post A Comment: