Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitoa maelezo juu ya uhamuzi wa kuhamishwa kwa Polisi waliokuwa wakifanya kazi kwenye kituo cha nyarugusu pamoja na mkuu wa kituo hicho. |
Mkuu wa wilaya Mwalimu Kapufi akiomba baraza la madiwani limpe ushirikiano katika kutekeleza uwajibikaji kwa wananchi. |
Madiwani wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya alipokuwa akiwaomba kushirikiana nae. |
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga akihaidi kuendelea kushirkiana na Mkuu wa wilaya . |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Geita,Barnabas Mapande akielezea juu ya madiwani kushiriki katika swala la ulinzi na usalama kwenye maeneo yao. |
Wawakilishi wa vyama vya siasa wilayani Geita ,wakisiliza kile ambacho kilikuwa kikiwakilishwa. |
GEITA :Serikali wilayani
Geita imewaondoa askari polisi wa kituo cha polisi Nyarugusu akiwemo mkuu
wa Kituo hicho, kwa kile kinachodaiwa kushindwa kuwajibika katika tukio
la ujambazi lilotokea Oktoba 14 mwaka huu baada ya mfanyabiashara wa dhahabu kuvamiwa
nyumbani kwake.
Akizungumza katika kikao
cha kuwasilisha taarifa za kata kwenye baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya
Geita Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman
Kapufi amesema askari hao walishindwa
kufika eneo la tukio kuwasaidia wananchi ikiwa ni mita chache kutoka kituo cha
polisi hali ambayo ilisababisha kutokea kwa ujambazi.
“Wamevamiwa saa sita ya
usiku hatua mia 200 kutoka kituo cha polisi wamepigiwa polisi simu zinaita na
walichelewa kufika katika tukio hali hii ilionekana ni makusudi nilifika na
kamanda wa polisi wa wilaya nimeagiza wale polisi wote waondolewe mara moja na
mkuu wao wa kituo”Alisisitiza Kapufi
Diwani wa kata ya
Nyarugusu,Swalehe Juma ameelezea kuwa kutokana na jeshi la polisi kushindwa
kuwahi katika tukio hilo wananchi walimwomba mkuu wa Wilaya kuwaondoa askari
waliopo kituoni hapo kwani wameonekana kushindwa kuwa waangalizi wa mali na
usalama wa raia.
Hivi karibuni watu saba (7)
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na nondo, marungu na mapanga walivamia
nyumbani kwa mfanyabiashara wa dhahabu Majaba Masanja mkazi wa Nyarugusu
wilayani Geita na kuchukua dhahabu gramu
860 na kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni sabini (70).
Imeandaliwa na Madukaonline na Adelina Ukugani.
Post A Comment: