Bukombe. Idadi ya wanafunzi wanaotarajiwa kuandikishwa kuanza darasa la
kwanza na elimu ya awali katika Kata ya Bulangwa wilayani Bukombe mkoani
Geita huenda ikaongezeka kutoka asilimia 60.4 ya mwaka huu hadi 81
kutokana na mwamko wa wazazi.
Mratibu Elimu Kata ya Bulangwa, Dunkani Ruzige aliimbia Mwananchi juzi
kuwa mwaka huu, zaidi ya wanafunzi 1,863 waliandikishwa katika shule
zilizoko kwenye kata hiyo, idadi inayotarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya
asilimia 20 mwakani.
“Wazazi wengi wamepata mwamko wa kuwaandikisha watoto wao hasa baada ya
Serikali kuanza kutekeleza Sera ya Elimu ya Msingi Bure,” alisema
Ruzige.
Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Mariko Nsoro aliwataka wazazi na walezi
wanaotarajia kuwaandikisha shule watoto wao kufanya maandalizi mapema
kwa kuwanunulia sare na mahitaji mengine kama madaftari na kalamu.
Navigation
Post A Comment: