Akizungumza Katika Kikao Cha Bodi Ya Barabara Mkoani
Hapa Mbunge Wa Geita Mjini Constatine
Kanyasu,Amesema Kuwa Kumekuwepo Na Kero Nyingi Kutoka Kwa Wananchi Kutokana
Na Kuharibiwa Kwa Miundo Mbinu Tangu
Kuanza Kwa Ujenzi Wa Barabara Hiyo Na Kwamba Imechukua Muda Mrefu Hali Ambayo
Imepelekea Kuwa Na Wasi Wasi Na Mkandarasi Ambae Anajenga Barabara Na Kwamba Yawezekana Uwezo Wake Kuwa Ni Mdogo.
“Tunamashaka na mkandarasi huyo kwani ni miezi mitatu
sasa tangu ujenzi huanze lakini bado hatuoni jitihada zikifanyika katika
kumaliza ujenzi huo mimi nafikilia sisi kama bodi tuje twende tukajione namna
ambavyo ujenzi huo unasua sua.”alisema Kanyasu.
Kutokana Na Swala Hilo La Barabara Mwenyekiti Wa Bodi
Hiyo Ambae Ni Mkuu Wa Mkoa Wa Geita,Meja Jenerali Mstafu Ezekiel Kyunga
Amefafanua Kuwa Ni Wajibu Wa Mkandarasi Kumaliza Ujenzi Huo Katika Wakati
Uliopangwa Hili Kupunguza Changamoto
Ambayo Wananchi Imekuwa Ikiwakabili Katika Eneo Hilo.
Akijibu Hoja Hiyo,Msimamizi Wa Barabara Hiyo
Mwandisi Kepucheki Mango,Ameeleza Changamoto Ya Kutokukamilika Kwa Wakati
Ujenzi Huo Ni Kutokana Na Kukutana Na Mwamba Kwa Baadhi Ya Maeneo Wakati Wa
Ujenzi Huo .
“Ujenzi wa barabara umechelewa kutokana na kukutana na
mwamba mgumu wakati wa ujenzi wa barabara hiyo na kwamba kwahiyo uchimbaji
umechukua muda mrefu lakini kwasasa mkandarasi ameongeza vifaa vya kazi na
anatarajia kuanzia December hataanza kuweka rami”alisema Mango
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE
Post A Comment: