Mkurugenzi wa halmashauri wa mji Mwandisi Modest Aporinali akielezea juu ya taarifa za kusimamishwa kwa mwalimu mkuu shule ya sekondari kasamwa.
GEITA:Siku chache kufuatia kusambaa kwa taarifa katika mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari
kuripoti kuhusu kuvuliwa madaraka kwa Mkuu wa shule ya Sekondari Kasamwa, Madukaonline imefanikiwa
kufika shuleni hapo lengo ni kutaka
kujua ukweli juu ya taarifa hizo ambazo zimetokana na itikadi ya vyama vya
kisiasa.
Madukaonline imezungumza na Mkuu wa
shule hiyo, Mwl Denis Otieno ,ameelezea kuwa chanzo cha kuvuliwa madaraka yake
na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm)
Mkoa wa Geita Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma ambaye pia ni
mbunge wa Geita vijijini ni kutokana na msimamo wake kupiga marufuku kikundi
cha wananfunzi cha Magufuli Clabu kufanya sherehe za kuagana(mahafali) shuleni
hapo hali ambayo ilipelekea Msukuma kumwagiza
mkurugenzi wa halmashauri ya mji kumshusha madaraka au
kumwamisha kabisa katika Mkoa ambao yeye ni mwenyekiti.
Mwalimu Audax Paul anadaiwa kuwa
mlezi wa Magufuli Klabu shuleni hapo alikana kwamba yeye sio hajihusishi na
maswala ya chama.
“Mimi ninachofahamu wanafunzi
walichangia fedha kwa ajili ya sherehe ya hapa shuleni na lengo lilikuwa sio
kufanya sherehe ya Magufuli Klabu ninachojua vijana wengi wa hapa kasamwa wapo
kwenye hii Klabu ya Magufuli na lengo lilikuwa ni kumuunga mkono Rais Magufuli
ili apite kwenye uchaguzi hayo mambo mengine mimi siyafahamu”alielezea Audax
Hata hivyo madukaoline imebaini kugawanywa kwa wanafunzi wa kidato
cha nne ambao wanatarajiwa kuanza kufanya
mitihani ya taifa mwezi wa kumi na moja (11)
tarehe moja(1) mwaka huu, ambapo baadhi yao wapo kwenye Magufuli Klabu na
wengine hawapo.
Willson Lugema ni mwanafunzi wa
kidato cha nne shuleni hapo amesema kuwa kulikuwa na vitisho kutoka kwa mwalimu
ambae ni mlenzi wa Klabu hiyo kuwa kama wasingechangia wangelifelishwa na
kwamba wale ambao waliunga mkono harakati hizo wao wangeweza kufaulu hali
ambayo ilipelekea kuingia kwa wasi wasi mkubwa kutokana na maneno ambayo
walikuwa wakiambiwa na wanafunzi ambao walikuwa wapo klabu hiyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa
Geita, Mwandisi Modest Apolinary, ameelezea kuwa hadi sasa bado hawajatoa barua
ya kumshusha cheo mwalimu huyo, na kwamba ameunda tume ya kuchunguza mwenendo
na nidhamu ya shule hiyo na pindi watakapokuwa wamebaini matatizo yaliyopo ndio
watatoa maamuzi ambayo yatakuwa na ushahidi wa juu ya swala la nidhamu shuleni
hapo na kwamba mkuu wa shule ni vyema akaendelea na majukumu yake ya kikazi ya
kila siku hadi pale watakapokuwa wamemaliza uchunguzi wao.
Shule ya sekondari kasamwa iliyopo halmashauri ya Mji wa Geita
iliazishwa mwaka 2004 na sasa ina jumla ya
wanafunzi 996 kuanzia kidato
cha kwanza hadi cha nne na kati yao waliojiunga na Magufuli klabu ni zaidi ya
wanafunzi 60 ambao walifanya mahafali nje ya shule oktoba 08 mwaka huu.
Imeandaliwa na Madukaonline.
|
Post A Comment: