MWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA SHINDANO LA MAPISHI FREDY OISSO AMEONDOKA LEO NCHINI KWENDA MAREKANI
MWAKILISHI kutoka nchini Tanzania katika shindano la Upishi duniani yanayotarajiwa kuanza Novemba 8-15 ameondoka mchana huu kuelekea nchini Alabama kwa ajili ya kwenda kuhakikisha anarudi na ushindi.
Fred Uisso ni mwakilishi pekee kutoka bara la Afrika kupitia baa ijulikanayo kama Club Afrikando ameweza kuingia katika fainali hizo kwa mara ya kwanza mwaka huu ambapo hatua ya awali iliweza kushirikisha nchi 54 duniani kukiwa na washiriki zaidi ya 3700.
Akiongea kabla ya kuondoka, Uisso amesema kuwa kitu pekee anachoweza kusema kuwa kila analolifanya anamuweka mungu mbele na watanzania wajue kuwa nimeenda kuwakilisha nchi na sio mtu mmoja kwahiyo matumaini makubwa ni dua zao kuniombea nifanikiwe kurudi na kombe pamoja na kitita cha hela.
Uisso ameweza kuingia katika vinyang'anyiro viwili tofauti, anawania World Stake Championship inayoshirikisha washiriki 50 pamoja na World Chef Championship ya washiriki 21 ambapo kutakuwa na mashindano ya kupika aina mbalimbali za vyakula ikiwemo vyakula vya asili kutoka nchini kwako.
Kumuweka mungu mbele, kupenda kitu anachokifanya pamoja na nidhamu kimemfanya Uisso kuwa mwakilishi pekee barani Afrika na kutokana na juhudi zake anazozionyesha kampuni ya Red Gold ikaamua kudhamini safari yake ya kuelekea Nchini Alabama.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Red Gold, Darsh Pandit amesema kuwa watanzania wengi hawajui kama kuna mashindano kama haya ila wao kama moja ya kampuni yenye kuhitaji kuona watu wanafanikiwa imeamua kudhamini safari hii na wataendelea kufanya hivyo kila wakati ukitegemea Uisso ni mwakilishi pekee kutoka Afrika na anaenda kupambana na nchi mbalimbali duniani.
Baadhi ya nchi washiriki wa mashindano hayo ni Visiwa vya Haiti, Poturico, Ukraine, Canada, Brazili, wenyeji Alabama na nchi nyinginezo
Post A Comment: