SHULE ya msingi Butwa iliyopo katika kijiji
hicho ndani ya kisiwa cha Izumacheli ziwa
Victoria upande wa Wilaya ya Geita inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu wanawake, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya
elimu kwa mtoto wa kike.
Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1983 na sasa
ina umri wa miaka 33 ikiwa ni shule ya pili katika kata ya Izumacheli,
imefahamika kuwa walimu wa jinsia hiyo wanapopangiwa kuripoti maeneo hayo
wamekuwa waonga wa kuishi kutokana na mazingira kuwa magumu kwao.
Leticia Zakayo ni mwanafunzi darasa la sita,
ni msichana pekee aliyethubutu kupaza sauti yake kwa niaba ya wenzake akiiomba
serikali kutatua changamoto ya walimu wa kike shuleni hapo.
‘’Mimi ni mwanafunzi wa darasa la sita tangu
nianze masomo yangu shuleni hapa sijawahi kumuona mwalimu wa kike..watoto wa
kike tunakabiliwa na changamoto nyingi sana mmoja wetu anapougua tunashindwa
kuwaelezea matatizo yetu hawa walimu wa kiume…kama mnavyojua tunakabiliwa na
changamoto nyingi,’’alisema Leticia zakayo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Omary Shabani
aliangazia changamoto zinazowakabili
watoto, ambapo alisema kuwa mtoto wa kike anapopata matatizo wamekuwa na
utaratibu wa kusaidiana wao kwa wao.
“Ni
kweli changamoto hii imekuwepo kwa muda mrefu ni wakati wa serikali kulitizama
hili kwa mapana yake watoto hawa hawako huru sana pindi wanapopatwa na shida,
wanapokumbana na changamoto tumekuwa tukiwatafuta wanafunzi wakubwa
wanasaidiana,’’alisea mwalimu Mkuu.
Mwalimu Herman Kapufi ni mkuu wa Wilaya ya
Geita wa kwanza kuitembelea shule hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 33 iliyopita
ambapo katika ziara yake alipoitembelea jana alikumbana na changamoto hiyo na
kuahidi kuwa kufikia januari mwakani shule hiyo itakuwa na walimu wa kike.
Imeandaliwa na Madukaonline.
Post A Comment: