Kuelekea mchezo wa watani wa jadi katika
jiji la London nchini England maarufu kama dabi ya London ya Kaskazini
kati ya Arsenal watakaowakaribisha Tottenham Hotspurs katika uwanja wa
Emirates siku ya Jumapili, wenyeji wa mchezo huo wamepata ahueni baada
ya wachezaji wake wanne wa kikosi cha kwanza ambao walikuwa majeruhi
kupata nafuu ya majeraha yao mna kwamba sasa wanaweza kujumuishwa katika
katika kikosi kitachocheza mchezo huo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana leo
zinaonyesha kuwa Theo Walcot, Sant Carzola, Hector Bellarin na Nacho
Monreal ambao wote walikosekana katika mchezo uliopita wa ligi ya
mabingwa barani ulaya dhidi ya Ludogorets Razgrad mbapo Arsenal
walishinda kwa magoli 3-2 wakitokea nyuma baada ya kutanguliwa kwa mabao
2, wanarejea baada ya kuonekana afya zao zikiimarika.
Arsenal wamepoteza mchezo mmoja pekee
toka ligi kuu ilipoanza baada ya kupoteza 4-3 dhidi ya Liverpool katika
mechi yao ya ufunguzi wa ligi, na baadae kutoka sare na mabingwa
watetezi Leicester City na timu ya Midlesbrough huku wakishinda mecchi
zilizobaki na kufikisha pointi 23 pamoja na viongozi wengine wa ligi
Manchester City na Liverpool.
Mechi ijayo ni muhimu kwa pande zote
mbili kwa kuwa ni mechi ya watani wa jadi lakini pia ni mechi inayowapa
nafasi kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi nchini England. Timu zote
zinaonekana kufanya vizuri katika michezo yao na wachezaji wa Arsenal
wanaorejea wamekuwa chachu ya kufanya vizuri kwa klabu yao ya Arsenal
Post A Comment: