CHELSEA CHALIIII,YAKUBALI KICHAPO TOKA KWA TOTTENHAM SPURS

Share it:



Magoli mawili ya kiungo mshambuliaji Raia wa Uingereza mwenye asili ya Algeria Dele Alli yametosha kuipunguza kasi Chelsea kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Chelsea imepoteza mchezo wake dhidi ya Tottenham Spurs baada ya kutandikwa jumla ya mabao 2-0 kwenye uwamja wa White Hart Lane Mjini London alikuwa Dele Alli aliwanyanyua mashabiki wake dakika ya 45 akifunga bao la utangulizi kwa wenyeji hadi mapumziko Spurs walikuwa mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko huku Chelsea wakiingia na kasi ya kutaka kusawazisha hata hivyo juhudi zao zilizimwa dakika ya 54 Dele Alli alifunga bao la pili kwa Spurs.
Baada ya kupigwa bao la pili Chelsea walipanic na kuanza kucheza Mpira wa nguvu na ubabe hadi mwamuzi anamaliza Mpira Spurs wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-0.
Na Matokeo hayo yameifanya Spurs kuchupa hadi nafasi ya tatu wakiwa na pointi 42 huku wapinzani wao wakubwa wa jiji la London Arsenal wakishuka hadi nafasi ya tano wakiwa na pointi 41 wakati Chelsea wamebaki kwenye kilele mwa Ligi wakiwa na pointi 49 huku wakiwa wanawazidi Liverpool pointi tano kwani wana alama 44.
screen-shot-2017-01-05-at-3-09-35-am
Share it:

michezo

Post A Comment: