Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT – Wazalendo Anna Mghwira amedai
kuwa harakati za kudai haki za wanawake na usawa wa kijinsia zimerudi
nyuma kwa kias kikubwa katika kipindi hiki cha uongozi wa wamu ya tano.
Amesema hali hiyo inatokana na kutozingatia baadhi ya madai muhimu ya wanawake.
Mghwira amesema kuwa miaka kumi iliyopita harakati za wanawake zilipiga
hatua kubwa kwa kuwa serikali ilitekeleza suala hilo takribani asilimia
30 hususani uwakilishi katika nafasi za uongozi.
Amesema ajenda ya haki za wanawake inakosa nguvu kwa sasa kutokana na
kukosa haki ya kikatiba kuhusu haki ya usawa wa kijinsia ambayo
ilipendekezwa katika mchakato wa katiba mpya.
Aidha Mghwira asema licha ya kuwepo kwa jitihada kubwa zinazofanywa na
Rais Dkt. John Pombe Magufuli tangu alipoingia madarakani ikiwemo
kurudisha nidhamu kwa watumishi wa umma bado harakati za kumkomboa
mwanamke dhidi ya mfumo unaokandamiza haki na usawa zimesahaulika.
Post A Comment: