Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe,Luhaga Mpina akitoa maelekezo ya utunzaji wa mazingira wakati alipokutana na kamati ya ulinzi na usalama Mkoani Geita. |
Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe,Luhaga Mpina,akisalimiana na mfanyabiashara wa soko kuu la Geita,huku akiulizia bei ya maembe. |
Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe,Luhaga Mpina,akitelemka kutoka katika chanzo cha maji kinachofadhiliwa na mgodi wa dhahabu wa GGM kilichopo Nyakanga. |
GEITA:Kutokana
na kuwepo kwa uharibifu wa mazingira ambayo yamekuwa yakisababishwa na shughuli
za kibinadamu Serikali imesema kuwa haitamwonea haya mtu yeyote ambae ataonekana
kukiuka na kutofuata sheria na taratibu za usafi wa mazingira zilizowekwa nchini.
Hayo
yamesemwa na naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira
Mhe,Luhaga Mpina katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Geita.
Mh,Mpina
amesema kuwa sheria zimewekwa kwa ajili ya kusimamiwa na kwamba suala la usafi
ni jukumu la kila mtu na kwamba kutokana
na magonjwa ya milipuko ambayo yamekuwa yakijitokeza yamekuwa yakilirudisha
nyuma Taifa katika swala la maendeleo.
“Kiongozi
Mkuu wa nchi ameshatoa maelekezo sheria zimetungwa na Miongozo imeletwa siku za kufanya usafi zimewekwa lakini watu
hawafanyi usafi hili swala la usafi ni vita ambayo ni lazima tuipiganie kwa nguvu zote
kamwe hatutaweza kuwalazia damu wale ambao wanakiuka sheria za mazingira”Alisisitiza
Mpina
Hata
hivyo Naibu waziri ametembelea mtaa wa
Katoma ambapo wananchi wamemweleza kuwa hali ya eneo hilo sio nzuri ni kutokana na kwamba kuna eneo ambalo mgodi
umekuwa ukitiririsha maji kuelekea maeneo ya wananchi hali ambayo imekuwa
ikisababisha wananchi kuwa na hofu kutokana na kujaa kwa maji eneo hilo huku
wakigusia kuwepo kwa vumbi linalotokana na uchimbaji katika mgodi wa dhahabu wa
Geita. (GGM)
Kutokana
na malalamiko hayo kutoka kwa wananchi Mh,Mpina ametoa miezi mitatu ya
kuhakikisha wanakamilisha mazungumzo na kujua ni wapi mfereji utapita ili uweze kuelekezea maji yatakapopolekwa na kuondoa
kero kwa wananchi ambao wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu.
Imeandaliwa na Madukaonline.
Post A Comment: