Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe,Luhaga Mpina,Akizungumza na wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi ya mistu wa Geita na kutengeneza makazi katika maeneo hayo. |
Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe,Luhaga Mpina,akiangalia maeneo ambayo yamefyekwa na wananchi kwa lengo la kutengeneza makazi kwenye msitu wa hifadhi wa Geita. |
Wananchi wakimsikiliza ,Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe,Luhaga Mpina wakati alipokuwa akitoa maagizo ya kuondoka katika maeno waliyovamia |
Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe,Luhaga Mpina,akipatiwa maelezo kwenye sehemu ambayo imekuwa ikiwekwa kwaajili ya maji machafu yanayotumika kuchenjulia dhahabu |
Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe,Luhaga Mpina,akikagua eneo la maji machafu lililopo kwenye mgodi wa Busolwa. |
Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe,Luhaga Mpina,akimpongeza Mkurugenzi wa mgodi wa CS,Coronel Simba kwa kuweka mazingiara vizuri kwenye eneo la mgodi wake. |
Wananchi
wanaoishi kwenye maeneo ya hifadhi ya mistu
Mkoani Geita,wametakiwa kupisha maeneo hayo ndani ya siku kumi na nne (14).
Hayo
yamesemwa na naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira
Mhe,Luhaga Mpina wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu (3) Mkoani
Geita,alipotembelea hifadhi ya pori la mistu ya Geita na kukutana na wananchi
ambao walimwomba Mh,Mpina kuwapatia
maeneo ambayo wamevamia na kutengeneza makazi.
Wakizungumza
kwa nyakato Tofauti,wananchi hao wamemwomba naibu waziri Mpina kuangalia
uwezekano wa kuwaachia maeneo hayo kwani wengi wao hawajapenda kuvamia maeneo
ya hifadhi ya taifa ya misitu ni kutokana na ugumu wa maisha ni sababu ambayo
imechangia kushindwa kulipia kodi za nyumba kwa wananchi ambao wamevamia hifadhi
hizo.
Kutokana na
kilio hicho cha wananchi ikamlazimu
Naibu waziri Mpina,Kutoa maelekezo ya wananchi kufuata kanuni na sheria
zilizowekwa na bunge pamoja na nchi
ikiwa ni pamoja na kufika katika ngazi zinazohusika pindi wanapohitaji maeneo
kwa ajili ya makazi na kuacha dhana ya kuvamia maeneo ya hifadhi bila ya
taratibu.
“Sasa kilio chenu cha kuhusu kwamba mnahitaji kupatiwa
sehemu, hilo litakwenda kwa utaratibu mwenyekiti na mkurugenzi wa halmashauri
wapo hapa mnaweza kuwaona na wakawasaidi lakini sio kuingia kinyume na
kujichukulia maeneo bila ya ridhaa ya serikali kwa hiyo ninawaomba wananchi
wangu ondokeni kabla ya hizo siku kumi na nne (14) kumalizika sisi tumewekwa
kusimamia sheria endapo tukizivunja nadhani tunaweza kuadhibiwa pia hivyo
nawaomba sana mzingatie sheria”alisema Mpina.
Hata hivyo
mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa
Geita,Leornad Bugomola,amewashukia wakala wa mistu nchini (TFS )Kwa kushindwa
kuwaondoa wananchi kwa wakati hadi wanafikia hatua ya kufyeka na kuweka makazi
kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi.
“Hili swala
ni lazima tuliweke wazi mimi kama mwenyekiti wa halmashauri ya mji nimeshaagiza
mara nyingi na mimi mtu ninayemwagiza ni afisa misitu ninapomwagiza anashindwa
kuingia kwenye misitu na kudai kwamba kuna wakala wa misitu wanasema
asaiwaingilie kwenye shughuli kwa hiyo hili suala mimi siwezi kumung’unya
maneno wakala wa misitu ana matatizo
maana wanawaachia wananchi wanajenga ndio wanakuja kuwatoa baada ya kuwa
wameshajenga”alifafanua Bugomola
Naibu waziri
mh Mpina amemaliza ziara yake huku akiagiza baraza la mazingira nchini (Nemc) kufanya
ukaguzi katika migodi yote midogo lengo likiwa ni kuangalia suala la uhifadhi
na utunzanji wa mazingira katika migodi hiyo.
Imeandaliwa na Madukaonline.
Post A Comment: