Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Igunga REVOCATUS KUULI
amewasimamisha kazi Afisa Ugani wa kata ya Itunduma, Mtendaji wa kata na
mtendaji wa kijiji cha itunduma kwa madai ya kushindwa kutekeleza
majukumu yao katika kusimamia kilimo cha pamba.
Hatua hii imefuatia mara baada ya mkuu wa mkoa wa Tabora AGGREY MWANRI kufanya ziara wilayani humu ili kukagua mashamba ya Pamba na kubaini uzembe mkubwa unaofanywa na viongozi hao alipojionea maotea ya pamba ambayo yameota na kupaliliwa shambani kinyume cha sheria ya kilimo cha pamba inayowataka wakulima kung’oa na kuchoma maotea kabla ya kupanda pamba nyingine na kutokuchanganya mazao.
Hii haikuishia kwa viongozi tu mkuu wa mkoa akatoa maelekezo kwa wakulima ambao wamechanganya pamba na mazao mengine kuchukuliwa hatua.
Mkoa wa Tabora ni moja kati ya mikoa iliyopewa jukumu la kuzalisha mbegu bora ya pamba ambapo asilimia 94 ya pamba yote inayolimwa mkoani hapa hulimwa katika wilaya ya Igunga

Post A Comment: