Afisa Uhusiano wa TBL Group Amanda Walter akielezea namna TBL
inavyoendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kutokomeza ajali za
barabarani kupitia Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani.
Kamanda wa Kikosi hicho,Kamishna wa Polisi ,Mohammed Mpinga akifafanua jambo katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Kikosi jijini Dar es Salaam.
Katika mkakati wake endelevu wa kampeni za Usalama barabarani,Kampuni ya TBL Group imetoa msaada wa Bajaj 2 kwa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kwa ajili ya kuongeza nguvu za kusimamia usalama barabarani.
Bajaj
hizo zimekabidhiwa kwa Kamanda wa Kikosi hicho,Kamishna wa Polisi
,Mohammed Mpinga katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Kikosi jijini Dar es Salaam.
Akiongea kabla ya kupokea msaada huo,Kamanda Mpinga aliishukuru TBL Group kwa msaada huo
ambao alidai kuwa utapunguza adha ya usafiri kwa askari kutoka kikosi
chake watakapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kuimarisha usalama
barabarani .
“Tunawashukuru
TBL Group kwa kulivalia njuga suala la usalama kikamilifu bila kuchoka
kwa kuwa wamekuwa ni wadau wakubwa wa mapambano ya kutokomeza tatizo la
ajali za barabarani na wamekuwa wakiunga mkono kampeni hizi kwa kipindi
cha muda mrefu”.Alisema Kamanda Mpinga.
Kwa
upande wake Afisa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Amanda
Walter,alisema kuwa kampuni ya TBL inaendelea kuunga mkono jitihada za
serikali za kutokomeza ajali za barabarani kupitia Kikosi cha Polisi cha
Usalama Barabarani.
“Tutaendelea
kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na serikali kupitia Kikosi cha
Usalama Barabarani na wadau wengine kupunguza matukio ya ajali za
barabarani ambazo zimekuwa zikipoteza maisha ya watu wengi na wengine
wakibakia kuwa na ulemavu bila kusahau hasara mbalimbali zinazotokea
kutokana na ajali”Alisema Amanda.
Aliongeza
kuwa hivi sasa kampuni hiyo imekuja na mkakati mkubwa wa kuendesha
mafunzo ya kuhamasisha jamii Unywaji wa Kistaarabu “Tukiwa
kampuni inayotengeneza vinywaji vyenye kilevi tunalo jukumu pia
kuhamasisha jamii kutumia vinywaji hivyo vizuri ili utumiaji wake
usilete madhara mengine kwenye jamii”
TBL
imekuwa ikiunga mkono kampeni za usalama barabarani ambapo kwa kipindi
cha mwaka huu imekuwa mmoja wa wadhamini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama
barabarani iliyofanyika kitaifa mkoani Geita ambapo iliwezesha idadi
kubwa ya madereva kupima afya zao kupitia huduma ya Zahanati Mwendo pia
imekuwa ikiendelea kudhamini kampeni hizo kwenye ngazi za mikoa ikiwemo
kudhamini mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za
msingi.
|
Post A Comment: