VIJIJI 126 VYAPATIA MRADI WA UMEME MKOANI SHINYANGA

Share it:
 Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar
Kanyama, akizungumza kwenye kituo cha Kibaoni Singida

Mkuu wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kibaoni mkoani Singida, akitoa maelezo kwa wahariri
 Kituo cha Kibaoni mkoani Singida ambacho kilifanyiwa upanuzi chini ya mradi wa Backbone


Wanakijiji  wa vijiji 126 wanaopitiwa na mradi mkubwa wa umeme, Backbone wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga 
kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, wataunganishiwa umeme kwa kulipia kiasi
kidogo cha fedha shilingi elfu 27,000/-, tu, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi.Leila Muhaji, (pichani juu) amesema.

Bi,
Leila ameyasema hayo kwenye kijiji cha Igurubya, mkoani Shinyanga, wakati wa 
ziara ya wahariri wa vyombo vya habari kutembelea mradi huo, Desemba 22, 2016.

“Nia
ya Serikali, kupitia Shirika lake la Umeme nchini TANESCO, ni kuwapatia
wananchi wote huduma ya umeme, ambayo ni muhimu katika kuinua uchumi wa 
mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kwa kawaida gharama ya kuunganishiwa umeme kwa vijijini ni shilingi 177,000/- pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT.” Alisema.

Kwa kuzingatia hilo, kumekuwepo na juhudi mbalimbali za Shirika la Umeme,
TANESCO, kufikisha huduma ya umeme vijijini chini ya mradi wa Wakala wa
Usamabzaji Umeme Vijijini (REA), lakini kukamilika kwa mradi huu wa Backbone 
kutaongeza kasi ya kuwapatia wananchi huduma hii muhimu ya umeme na kwa bei 
nafuu.” Aliongeza. 

 Alisema, Serikali kupitia TANESCO imepiga 
hatua kubwa ya kuwafikishia umeme wananchi ambapo tayari karibu asilimia 45 ya 
wananchi wa Tanzania wamepatiwa huduma ya umeme.

Akizungumzia 
kukamilika kwa mradi huo wa Backbone uliojikita katika kujenga minara na njia 
za kusafirisha umeme pamona na upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza 
umeme, Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar.

Kanyama, alisema, mradi huo wa Backbone wa kusafirisha umeme wa msongo wa 
Kilovolti 400, na urefu wa Kilomita 670, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga 
kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, umekamilika rasmi Desemba 22, 2016 kwa 
kuwasha kipande kilichokuwa hakijakamilika cha kutoka Dodoma kwenda Singida.

Mradi 
huo ulianza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2013 na unafadhiliwa 
na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo umegharimu karibu 
shilingi Trilioni 1.

Kazi 
iliyokuwa ikifanywa ni pamoja na ujenzi wa minara mikubwa yenye uwezo wa kubeba 
nyaya 6, tatu kila upande tofauti na ile ya awali iliyokuwa na uwezo wa kubeba 
nyaya 2 tu moja kila upande. “Lakini pia kazi nyingine iliyokuwa ikifanyika 
chini ya mradi huu, ni upanuzi wa vituo vinne vya kupoza na kusambaza umeme, 
vituo hivyo ni kile cha Iringa, Zuzu, mkoani Dodoma, Kibaoni mkoani Singida, na 
Ibadakuli mkoani Shinyanga Shinyanga.” Alifafanua.
Share it:

matukio

Post A Comment: