FIGISU FIGISU ZATAWALA UCHAGUZI GEREFA

Share it:

Wajumbe wakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa GEREFA Salim Kurunge kwenye uchaguzi wa viongozi wa mpira mkoani Geita.

Mwenyekiti aliyepita Mkono wa kushoto na Makamu wake wakifatilia matokeo wakati yalipokuwa yanatangazwa.

Mwenyekiti wa uchaguzi ,Bernad Otieno akisoma matokeo ya uchaguzi.

Michael Wambura ambae ni kamishana wa shirikisho la soka Afrika akitoa ufafanuzi wa Rufaa iliyotolewa na mahakama.

Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Geita ,aliyechaguliwa Salum Kurunge akitoa neno la shukrani kwa wajumbe kumchagua tena.

Mwandishi Nguli Mkoani Geita ,Victor Bariety akifatilia kwa makini uchaguzi.





Chama cha mpira wa miguu Mkoani Geita,Kimefanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali hapo jana pamoja na kutawaliwa na figisufigisu kwa baadhi ya wagombea kuweka pingamizi la uchaguzi huo kutokufanyika siku hiyo na badala yake mahakama itangaze tarehe nyingine ya kufanyika.

Wagombea ambao waliokuwa wamekimbilia mahakamani kupinga uchaguzi huo usifanyike kwa madai ya kuhujumiwa kwenye rufaa yao waliyokata kwenda TFF baada ya kuenguliwa kwenye usaili wa kuteua wagombea na ambayo hadi siku ya uchaguzi ilikuwa haijajibiwa  ni Leornad Mnenge na Musuka Charles.
Hata hivyo matokeo ya rufaa yao yalirudi mnamo majira ya saa 4 usiku Desemba 20  wakati tayari wagombea hao walikwisha weka pingamizi kwenye mahakama ya wilaya ya Geita.
Baada ya mvutano wa hapa na pale baina ya wagombea hao na mwenyekiti wa uchaguzi huo,Bernad Otieno ambaye kitaaluma ni mwanasheria walikubaliana kuondoa pingamizi hilo mahakamani kwa walalamikaji kuandika barua ya kuondoa shauri hilo mahakamani.

Barua hiyo iliyoandikwa na Mnenge pamoja na Charles kwenda kwa hakimu wa mahakama ya wilaya ya Geita pamoja na mambo mengine  iliomba kutengua madai yao namba 250 ili taratibu za uchaguzi ziendelee .

“Naomba kutaarifu Mahakama yako tukufu kwamba sina nia ya kuendelea na shauri ya madai namba 250 kama ilivyonukuliwa kwenye kichwa cha habari hapo juu ninaomba kuondoa madai yangu pamoja na kuiomba mahakama ili kutekelezwa zuio lililotolewa zidi ya wadaiwa /wajibu maombi”Ilisomeka sehemu ya Barua hiyo.

Kufatia hali hiyo taratibu za uchaguzi zilizendelea na majira ya saa 10:20jioni mwenyekiti Otieno alitangaza washindi wa nafasi zilizkuwa zikiwaniwa  

Katika matokeo hayo aliyekuwa mwenyekiti wa GEREFA Mkoa Salum Kurunge alifanikisha kutetea kiti chake kwa mala nyingine  kwa kura  15 dhidi ya ishirini zilizopigwa.

Nafasi ya makamu mwenyekiti ilikwenda kwa Joseph Kabote,Katibu Mkuu Deus Seif,huku Pius Kimisha  akichaguliwa kuwa msaidizi wake.

Nafasi ya mtunza hazina iliachwa wazi kutokana na mgombea kutofika ukumbini huku  Idrissa Sued,Elias Manyama na  Domisian Kabalega, wakichaguliwa kuwa wajumbe wa kamati tendaji.

Aidha kwa aliyechaguliwa kushika nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF ni Elisa Mgisha na Saimon Shija kuwa mwakilishi wa virabu.

Imeandaliwa na Maduka online.



Share it:

michezo

Post A Comment: