Katibu tawala wa wilaya ya Geita,Thomas Dimme ,akitoa maelekezo kwa wajumbe wa mkutano huo. |
Wajumbe wakimsikiliza mkuu wa wilaya alipokuwa akitoa maelekezo ya kutumia fursa zilizopo katika maeneo wanayoyaongoza. |
Watendaji wa kata na Mitaa na maafisa tarafa wakifatilia kwa makini. |
Mkuu
wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi amewataka watendaji na maafisa tarafa wilayani humo
kutumia fursa zinazopatikana katika maeneo ambayo wanafanyia kazi ili
kuweza kujinufaisha ikiwa ni pamoja kufungua viwanda vidogo ambavyo vitaleta
faida katika jamii.
Hayo
ameyasema wakati wa kikao cha
wakurugenzi wa halmashauri ya wilaya na
mji,wakuu wa idara kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya maafisa tarafa na
watendaji wa kata ,ambapo ni moja kati ya mambo ambayo amewahimiza viongozi
hao baada ya kupata mafunzo mafupi ya
kuzitambua fursa na kuzitumia aliyoyapata nchini China hivi karibuni.
Mh
Kapufi,alisema kuwa wao kama watendaji
wana uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha
ya wananchi kwa kuandika ombi mradi ambalo wataliwasilisha kwa afisa mipango
ambae anaweza kuomba kwa shirika lolote kutengeneza kiwanda ambacho kitasaidia
wakulima wa mananasi na mazao mengine kuweza kuuza kwa bei nzuri katika kiwanda
cha kuchakata kitakachokuwa kimejengwa eneo husika ambalo litakuwa limepangwa.
“Mnaweza
kufanya andiko mkamletea afisa mipango ambae akashirikiana na mkurugenzi na
mkuu wa wilaya ambapo anaweza akaomba kwa SIDO na kusaidiwa na kisha hawa wakulima
na wafugaji viwanda hivi vinaweza
kuwasaidia kwani watauza mazao yao kwenye kiwanda ambacho kitawapa
faida”alisema Kapufi
Baadhi
ya watandaji wa kata ambapo wamesema kuwa wanaamini viwanda ambavyo vitajengwa
hususani vya mananasi vitawasaidia wakulima kuinua uchumi wao na kwamba
wataweza kusaidia mapato kuongezeka katika halmashauri zilizopo wilayani humo.
Hatua
hii inakuja ni baada ya kauli ya Rais Magufuli ya kutaka Tanzania kuwa nchi ya
viwanda na kwamba kutumia mali zilizopo kwa ajili ya kunufaisha wazawa lakini pia
kutoa ajira kwa baadhi ya watanzania wasio na kazi za kufanya.
Post A Comment: