DC GEITA AKUBALIKA KWA WANANCHI KUTOKANA NA UTENDAJI KAZI WAKE IKIWEMO SWALA LA KUSIKILIZA KERO NA KUZITATUA.

Share it:
Baadhi ya wananchi wa kata ya Katoro wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi wakati alipokuwa akizungumzia swala la ushiriki wa wananchi katika uchangiaji wa maendeleo katika kata hiyo.

Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Katoro ,Peter Janga akielezea namna ambavyo wamekuwa wakitoa huduma ya matibabu ya wagonjwa ambao wanatumia bima ya afya kama ambavyo swali liliulizwa na moja kati ya wananchi ambao walikuwepo katika mkutano huo.

Mganga mkuu wa wilaya ya Geita Raphael Mhina ,akiwaeleza wananchi hali ya dawa ilivyo kwasasa katika wilaya ya Geita.

Wananchi wa kata ya Katoro wakifatilia kwa makini kile ambacho kilikuwa kikijili katika Mkutano huo.

Wananchi wa mamlaka ya mji Mdogo wa Katoro Mkoani Geita, wamekubali utendaji wa kazi alioanza nao Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Heriman Kapufi wa kuzunguka na kuzungumza na wananchi kusikiliza kero zao na  kuzitatua swala ambalo ni kinyume na viongozi baadhi ambao wamepita hapo nyuma.

Wakizungumza   katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa Katoro wananchi hao walisema kuwa Mkuu huyo wa wilaya ameletwa na mwenyezi Mungu hivyo wanaimani naye kuwa atakuwa mstari wa mbele kutatua kero zinazowakabili.

Katika Mkutano huo wananchi walitoa changamoto mbalimbali, huku sekta ya afya ikilalamikiwa na wananchi wengi ambapo akina mama walisema wamekuwa hawapatiwi huduma inayotakiwa.

“Mkuu wetu wa wilaya tukueleze tu, sisi hatuna mashaka na wewe kwa jinsi ulivyo umekuwa na hofu ya Mungu tunajua maendeleo kwa wilaya yako ya Geita yatakwenda kwa kasi viongozi wengi hapa Geita wamekuwa wakitusimamia na kututofautisha  kutokana na hali zetu za kimaisha mambo yaliyokuwa yakikwamisha kutokana na migongano  watu wa Katoro tulikuwa wachangiaji wakubwa katika maendeleo ya kata yetu,’’ alisema mkazi wa katoro


DC Kapufi ambaye amekuwa akimtanguliza Mungu katika vikao vyake na mikutano  mbalimbali ya wananchi, huku akiuhubiri upendo kwa wananchi jambo ambalo limewavutia wengi huku wakiahidi kumpa ushirikiano ili kuijenga Katoro na Geita kwa ujumla ambayo imetawaliwa na itikadi za kisiasa  huku miradi mbalimbali ya maendeleo ikikwamishwa na baadhi ya wanasiasa.
Share it:

habari

Post A Comment: