KUMI NA NNE WAFUKIWA NA SHIMO KWENYE MGODI WA RZ NYARUGUSU

Share it:
Shimo lililojifukia jitihada zikiendelea za uokoaji

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita.Elisha Mugisha,akitoa maelezo namna ambavyo wanaendelea na jitihada za kuokoa

Kamisha msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Mhandisi Yahaya Samamba ,akifafanua namna ambavyo wameweza kuwasiliana na makapuni mengine ya uchimbaji wa madini kwaajili ya kutoa msaada kwa watu waliofukiwa

Moja kati ya wafanyakazi kwenye mgodi huo akielezea hali ilivyotokea na shimo lilivyojifukia

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,akiambatana na msemaji wa mgodi huo Frances Kiganga pamoja na kamanda wa zimamoto,Elisha Mugisha wakielekea kwenye eneo ambalo shimo limejifukia. 

Eneo la shimo likiendelea kuchimbwa

Jitihada zikiendelea za uokoaji

Baadhi ya waokoaji wakisemezana namna ya kuokoa

Shughuli zikiendelea 


Mwanasheria na msemaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya RZ  Frances   Kiganga ,akielezea chanzo cha mgodi huo kujifunika. 






WATU kumi na nne(14)mmoja akiwa ni Raia wa China wamefukiwa na udongo usiku wa kuamkia leo  majira ya saa saba usiku (7:00)wakiwa wanaendelea na majukumu yao ya uchimbaji  kwenye kampuni ya RZ Iliyopo kijiji cha Nyarugusu  wilayani  na Mkoa wa  Geita.

Sababu za kuporomoka udongo  ni kutokana na mgodi kuchimbwa  zamani na Wajerumani hivyo kupelekea baadhi ya maeneo hayo kuwa na nyufa na vyuma kushindwa kushikilia udongo wa juu hali ambayo imepelekea kuzidiwa na mwisho wa siku kuporomoka.

Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita,ikiongwaza na mkuu wa Mkoa huo Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga  imefika katika Mgodi wa RZ kuangalia  na kujionea zoezi la ukoaji  .

Kamisha msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Mhandisi Yahaya Samamba ,ameelezea  kuwa jitihada ambazo zimefanyika ni kuwasiliana na migodi iliyopo karibu na eneo hilo  na pia wameshaomba msaada Kahama na kwenye mgodi wa GGM kupatiwa vifaa vya uokoaji ili zoezi hilo liwezekufanikiwa kwa urais zaidi.

“Jitihada ambazo tumezifanya hadi sasa tumeomba msaada kahama na kwenye mgodi wa Geita,kupatiwa vifaa ambavyo vitasaidia kwa wepesi zoezi hili la uokoaji ingawa tumeshapata vifaa vingine kutoka kwenye mgodi wa Busolwa”Alisema Samamba.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita.Elisha Mugisha,amesema kuwa eneo la chini ambalo limefukiwa na udongo ndio ambalo  kwa sasa wanaendelea kulitanua ili sehemu hiyo iwe kubwa watu waweze kupita.

“Eneo lote lile la chini limefukiwa na udongo lakini kule chini kunaonekana kuna  sehemu za kwenda pembeni ingawa limefukiwa lakini chini kunauhimala  kunauwezekano kule chini wale watu wapo hai na wamepelekewamipira ya hewa na kazi inayofanyika ni kutanua eneo ambalo litasaidia kuwatoa watu hao”tumekwisha kupeleka mipira

Mwanasheria na msemaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya RZ  Frances   Kiganga  ameelezea kuwa  chanzo kikubwa ni mashimo ya zamani kwani udongo unapotikisika umekuwa ukisababisha baadhi ya nyufa kuendelea kupata shida.

Baadhi ya wafanyakazi  wa kampuni hiyo Charles Julius Na Robert Stanleyambao wameeleza kuwa mida ya saa saba usiku duara lilinza kushuka taratibu na baada ya hatari hiyo walipewa taarifa ya watu ambao walikuwa chini kupandisha juu lakini hata hivyo jitihada hizo hazikuzaa matunda.

 Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amewataka wanaosimamia zoezi la uokoaji kuongeza nguvu ya uokozi .
Hadi Madukaonline inaondoka kwenye eneo la tukio akuna mtu yoyote ambaye ameokolewa ingawa jitihada bado zinaendelea kwa kuomba mashirika kuweka msaada zaidi wa uokoaji.

IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE



Share it:

matukio

Post A Comment: