Meneja wa Mgodi huo,Guixue Liu,akiwa na Mwanasheria wa Mgodi Huo Frances Kiganga wakiangalia namna kazi zinavyoendelea kwenye mgodi.
SAKATA la
watu wawili wanaodaiwa kupigwa na raia
wa kigeni wa China akiwemo aliyelazwa katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa
wa Geita limechukua sura mpya baada ya kubainika chanzo chao cha kupigwa ni
kuiba mawe yanayodhaniwia kuwa na dhahabu na maji walipokuwa wakifanya kazi katika mgodi wa wa dhahabu unaomilkiwa na kampuni ya RZ
uliopo katika kijiji cha Mawemeru wilaya na mkoani Geita na siyo kutokana na
madai kupandishwa mishahara.
Tukio hilo
limetokea Januari 19 wakati wa zamu ya usiku baada ya mfanyakazi Benedict
Lumimi Maduhu kudaiwa kukamatwa akiwa na mawe yanayodhania kuwa na dhahabu
ndani ya mgodi huo wakati akiwa zamu usiku
na baada ya kukamatwa rafiki yake wa karibu na ndipo rafiki yake wa Karibu Elisha Silivester [26] ambaye naye
anatuhumiwa kwa kuiba maji alifanikiwa
kukimbia hadi kituo cha polisi cha Nyarugusu kutoa taarifa kuwa yeye na mwenzake walikuwa wakipigwa na
wachina baada ya kudai waongezewe mshahara.
Akithibitsha
tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema wafanyakazi Bedeicto
Lumimi Maduhu walikamatwa na polisi kutoka ndani ya mgodi huo baada ya kukuta
tayari amekamatwa na kufungwa kamba na
wafanyakazi wengine wa mgodi huo tayari kwa kumpeleka kituo cha polisi cha Nyarugusu
pamoja na mawe yanayodaiwa kuwa na
dhahabu .
Ameongeza
kuwa Elisha Silvesta anayedaiwa kuiba maji yeye ndiye aliyekimbia na kutoa
taarifa kituo cha polisi baada ya kufanikiwa kutoroka kabla ya kukamatwa na polisi baada ya kufika eneo
la tukio waliwachukuwa watuhumiwa Benedicto
pia wafanyakazia baadhi wa mgodi huo hadi kituo cha polisi kwa mahojinao
ikiwani pamoja na kuwahoji baadhi ya
wafanyakazi wa mgodi huo akiwemo Elisha mwenywe.
''Taarifa rasmi za uchuguzi ni kuwa chanzo cha kupigwa
kwao ni kutuhumiwa kwa wizi wa mawe
yanayodhaniwa kuwa na dhahabu na maji kama nilivyoeleza sisi
kama polisi pia baada ya kutokea malalamiko hayo kutoka kwa watuhumiwa pia wanaotuhumiwa tulichukua jukumu la
kuwakamata na kuwahoji na kinachoendelea
sasa ni mchakato wa kukusanya ushahidi
kwa hatua za kisheria hivyo
chanzo ni cha wao kupigwa ni kutuhumiwa na siyo madai ya nyongeza za
mshahara”alidai Mponjoli.
Hata hivyo
polisi imebainisha wazi kuwa zipo changamoto kwa baadhi ya watu kujenga hoja
zinazolenga kujipatia
fedha kutoka
kwa wachina kwa kujenga hoja ya kupigwa
na kujeruhiwa vitendo alivyodai polisi haina budi kuyafanyia kazi kwa umakini
madai hayo kwa vile tayari ipo mifano ya
matukio ambayo yaliwasilishwa lakini yakaisha kwa walalamikaji kudai pesa na kutelekeza kesi zao.
Ametoa mfano
tukio lililtokea julai 6 mwaka jana la Masanja
Shilomero[25] mkazi wa kijiji Nyamitondo
kudai kushambuliwa na wajiri wake ambao ni raia wa china na kufunguliwa
kesi namba CC/278/2016 mlalamikaji aliitelekeza kesi hiyo baada ya kudaiwa alikuwa
ameomba na kupewa fedha kutoka kwa walalamikiwa
na kuitelekeza kesi yake.
Kesi hiyo kushindwa kuendelea na siyo kwamba
imetelekezwa na polisi,na tukio jingine amelitaja kuwa ni mchimbaji Richard
Kasubi anayelalamikiwa na baadhi ya watu wanaodaiwa kufanya kwake kazi ya kushusha
mifuko ya saruji kutoka katika gari kuiweka katika
ghala lake
badaye walidai kudhurika hata hivyo tayari inadaiwa walilipwa pesa na
mlalamikiwa huyo baada ya kutaka malipo kwa ajili ya matibabu na baada ya kiasi
cha shilingi 500,000 wanachodaiwa kupewa kukimaliza walianza tena kudai upya na
hivyo kuibua mgogoro.
kutokana na
uwepo wa mazingira ya aina hiyo polisi wanatakiwa kufanya kazi kwa umakini ili
kutenda haki kwa pande zote na kuwa Benedicto na wenzake tayari amefunguliwa
kesi ya wizi wa mawe yanaodhaniwa kuwa
na dhahabu katika kituo cha polisi cha Nyarugusu na upelelezi wake unaendelea
ikiwemo wanaodaiwa kuwapiga nao wamefunguliwa kesi na inachunguzwa.
Awali
akizungumzia matukio hayo Meneja wa mgodi huo wa RZ Gui Xue Liu kupitia msemaji
wa kampuni hiyo Francis Beatus Kiganga amesema vitendo vya wizi kwa wafanyakazi
wanavyofanya na kisha kuwageuzia kibao kunaweza kuwakatisha tama kuwekekeza
katika sekta hiyo ya madini kwani imekuwa
ikiwapa usumbufu mkubwa.
Amesema kwa
kawaida wao wamekuwa wanapowakamata watuhumiwa
huamua kuwafukuza kazi badala ya kuwapeleka
kwenye
vyombo vya sheria ili kuepuka kupoteza muda na usumbufu na watuhumiwa kutumia
mwanya huo huwageuzia kibao hatua waliyodai inaonekana kuwaathiri na kuiomba
serikali kulifanyia kazi kwa umakini wimbi hilo la wachina kutuhumwia kupiga
watumishi.
Mganga wa
zamu katika hospitali hiyo Elias Hambuhambu amethibitisha juzi jioni kwa Elisha
Sivesta kulazwa hospitalini hapo kwa madai ya kupigwa na kuwa hata hivyo hali
yake ilikuwa inaendelea vizuri na alikanusha uwepo uvumi wa kujeruhiwa sehemu
za siri za majeruhi huyo kwani alikuwa amewekewa mpira wa haja ndogo kama hatua ya kawaida kwa
wagonjwa wanaolazwa wanaokuwa na madai ya kusikia maumivu ya mwili.
Baadhi ya
wafanyakazi wa mgodi huo wakiwemo Amani Silivesta na Annicent Masanja walidai
mwenzao elisha aliondoka kwenda kuropiti Kituo cha polisi akijihami baada ya
Benedicto kukamatwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu wakati
alipokuwa zamu ya usiku na waliondoka na
Polisi baada ya yeye kwenda kutoa taarifa na wakati huo wote hakuwa amepigwa na madai ya kupigwa yamejitokeza
siku mbili baada ya kutokea uhalifu huo hivyo kuibua sintofahamu.
Akizungumzia
tuhuma hizo Elisha Silvesta akiwa wodini alimolazwa juzi katika hopitali teule
ya mkoa wa Geita alikiri kuwa chanzo cha wao yeye na Benedicto kupigwa ni kutuhumiwa
yeye kuiba maji na mwenzake Benedicto
kuiba mawe yanaodhaniwa kuwa na dhahabu na baada ya kufanikiwa kukimbia alikwenda kutoa
taarifa kituo cha polisi Nyarugusu kuwa mwenzake Benecto Lumimi Maduhu alikuwa
amefungwa kamba akipigwa bakora na wachina ili kujihami.
Imeandaliwa na Madukaonline. |
Post A Comment: