Baadhi ya samaki waliokamatwa wakionekana wakati wa zoezi la kuwatambua samaki ambao ni wakubwa na wadogo. |
Gari lenye Namba T 199 AUN Toyota Hiace, ambalo lilikuwa
likiendeshwa na Nicodemus James mkazi wa Katundu mjini Geita limekamatwa
na maafisa Uvuvi wa halmashauri ya wilaya ya Geita wakati
likisafirisha samaki wachanga wenye inchi moja na nusu mpaka mbili wakiwa
kwenye madumu, mifuko na mabox wakiwa na kilo elfu 11896
wenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 11.8.
Pamoja na jitihada za Serikali Wilayani na Mkoani Geita kuwa na vita kubwa ya kutokomeza mtandao wa wavuvi haramu katika
mwambao wa ziwa Victoria lakini bado kuna
changamoto kwa baadhi ya
wafanyabiashara wa samaki, ambao wanaendesha biasahara hiyo kinyume
na sheria ya uvuvi ya namba 22 ya mwaka 2009 kwa kuendelea kuuza samaki ambao hawajakidhi viwango mara
baada ya kutoka kulangua kwa wavuvi.
Afisa mfawidhi wa uthibiti
ubora wa samaki na usimamizi wa rasimali na uvuvi kanda ya Mkoa wa
Geita,Shafii Ramadhani,alisema kuwa uvuvi haramu umeendelea kuiletea hasara
kubwa serikali kutokana na kiwango cha samaki wanaovuliwa kutokufikia wakati
wake sahihi wa kuvuliwa na tatizo kubwa lipo kwa baadhi ya wavuvi ambao
wamendelea kutumia makokoro ambayo yameendelea kuzuhiliwa.
“Kwa ujumla hata sisi tunasikitishwa na vitendo ambavyo
vimeendelea kufanywa na baadhi ya wavuvi kuendelea n dhana haramu ambazo
tumeendelea kuzuhia swala hili kwa mfano kama wafanyabiashara wakiacha kununua
hawa samaki hayupo mvuvi hatakae vua samaki hawa wachanga”Alisema Shaffi
Bw,Ramadhan ameongezea kuwa kukamatwa kwa mfanyabiashara ni
kutokana na kwamba yeye anakuwemo kwenye mlolongo wa Makosa kwani
kile ambacho kinafanyika sio uwonevu kwa wananchi nia ya serikali ni kuakikisha jamii
inanufaika na maliasili hiyo kwa kuzingatia kanuni zilizowekwa
. Kwa upande wao wafanyabiashara wa samaki,Paul Ndonge na Emmanuel Lukanga ,wameeleza kuwa lengo lao
sio kununua samaki wadogo sababu
zinazopelekea kununua samaki hao wadogo ni kutokana na kutokuwapata samaki
wakubwa pia wameiomba serikali kuweka nguvu zaidi kwa wavuvi ambao wanavua
samaki wadogo kwani wao ndio chanzo kikubwa cha kuendeleza biashara hiyo mbayo
imekwisha kuzuhiliwa.
Maeneo ambayo yanakabiliwa na uvuvi haramu katika mwambao wa
ziwa Victoria Wilaya ya Geita ni pamoja na Kata ya Senga, Nkome, kisiwa
cha Izumacheli na Mwalo wa Beach Chato Wilayani humo.
Post A Comment: