BREAKING NEWS: WACHIMBAJI SITA WAFUKIWA NA KIFUSI MARA

Share it:



HABARI zilizotufikia hivi punde zimeelza kuwa wachimbaji sita wa madini wanadaiwa kufukiwa na kifusi walipokuwa wakichimba madini kwenye mgodi wa Buhemba ulioko mkoani Mara.

Imeelezwa pia kuwa watu 11 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambapo wamekimbizwa katika Hospitali ya Butiama kwa ajili ya matibabu.

Global Publishers imefanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi ambaye amekiri kutokea kwa ajali hiyo.

“Ni kweli ajali hiyo imetokea leo, na hivi sasa nipo eneo la tukio. Kuhusu takwimu sahihi za watu waliofukiwa kwa sasa sina, mpaka uchunguzi wa jeshi la polisi utakapofanyika ndipo nitatoa ripoti kamili.” Alisema Kamanda Ng’anzi.

Tukio hilo ni la pili ndani ya kipindi kifupi ambapo siku za hivi karibuni, wachimbaji 15 walifukiwa na kifusi na kuokolewa baada ya siku kadhaa katika Mgodi wa RZ, Nyarugusu uliopo Nyarugusu mkoani Geita.
Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA LIPO IMARA KUDHIBITI UHALIFU NA MAANDAMANO APRILI 26

Jeshi  la polisi mkoani Geita , limewataka  wananchi  katika kuelekea   siku kuu ya pasaka

JOEL MADUKA