Kampuni ya ORICA ambayo inafanya kazi za kulipua miamba ya
dhahabu kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) na Buzwagi Imetoa vifaa tiba
kwenye kituo cha afya cha Nyakumbu kilichopo kwenye kata hiyo wilaya na Mkoa wa
Geita vyenye thamani ya shilingi Milion mbili(2,000,000)
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo ,Msimamizi msaidizi wa kituo cha Orica mhandisi Pascal Malugu,amesema kuwa walifikiria
kuwa sio vyema kwenye jamii ambayo wanafanyia kazi kutokutoa mchango wowote
ambao utasaidia jamii hivyo wakaguswa na kuamua kutoa vifaa tiba ambavyo
vitasaidia kutoa huduma za kiafya huku akitoa wito kwa makapuni mengine
kujitolea misaada mbali mbali.
“Leo hii si
mara ya kwanza katika jamii kutoa misaada kwani tulishawahi kutoa kifaa kingine
cha Eqbet kwenye hospitali ya Geita na
sisi tuliona sio vyema kutotoa misaada ambayo itasaidia jamii inayotuzunguka lakini niombe Mashirika na Makapuni mengine
kuguswa na kutoa misaada kwani hii ndio dini safi kuwasaidia ambao ni
wagonjwa”Alisema Malugu.
Hata hivyo
kwa upande wake msimamizi mkuu wa kampuni hiyo,Yahaya Puyaga ameelezea kuwa
wanaamini kuwa msaada ambao wameutoa utapunguza adha iliyokuwepo kwenye kituo
hicho na kwamba ni mwanzo tu kwani
wanajipanga kuendelea kutoa mchango zaidi
kwenye maeneo yaliyopo ndani ya Mkoa wa
Geita.
“Sisi kama
saiti ya Geita tulikaa wafanyakazi na
kuweza kufikiria kwamba je sisi kama sisi tunaweza kufanya kitu gani kwenye
jamii ili walau na sisi tuweze kuleta faida kwenye jamii inayotuzunguka ndipo
tulipoamua kuunda tume ya kufuatilia vituo vyetu vya afya vilivyopo kwenye
halmashauri ya mji mwisho wa siku tukajua kituo
cha Nyakumbu kina uhitaji mkubwa ndipo tulipoamua kutoa msaada huu wa
vifaa tiba”Alisema Puyaga.
Aidha mganga
mfawidhi wa kituo hicho,Abdallah Amiry Kiroboto amesema kuwa vifaa
walivyopatiwa vitawasaidia kurahisisha kazi na kwamba kwa sasa wataweza kupima
magonjwa ya kisukari kutokana na kupatiwa kifaa hicho huku akiomba msaada kwa
wadau wengine kufika katika kituo hicho na kuwasaidia kwani wana upungufu
mkubwa wa vifaa vingi vya kufanyia kazi.
Baadhi ya
wananchi ambao walikuwepo kwenye makabidhiano hayo wameishukuru kampuni hiyo
kwa moyo wa kujitolea huku wakiomba makampuni ambayo yamo ndani ya mgodi wa GGM
kuiga mfano wa kampuni hiyo.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: