VIROBA VYA MILION 140 VYASALIMISHWA NA WAFANYABIASHARA MKOANI MANAYARA

Share it:

Wafanyabiashara 13 wa Wilaya za Babati na Hanang’ Mkoani Manyara, wamesalimisha katoni 1,540 za pombe zilizofungashwa kwenye karatasi (viroba) zenye thamani ya sh140 milioni.

Wafanyabiashara hao walisalimisha katoni hizo za pombe za viroba kabla ya upekuzi ulioendeshwa na polisi, maofisa wa usalama wa Taifa, chakula na dawa (TFDA) na mamlaka ya mapato nchini (TRA).

Akizungumza jana na waandishi wa habari, kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Francis Massawe alisema wafanyabiashara hao walisalimisha wenyewe viroba hivyo bila kushurutishwa.


Kamanda Massawe alisema katika wilaya ya Hanang’ zilisalimishwa katoni 871 na kwa wilaya ya Babati zilisalimishwa katoni 669 na wafanyabiashara hao wanaopaswa kupongezwa kwa hatua hiyo.
Share it:

JOEL MADUKA

magazeti

Post A Comment:

Also Read

NFRA YAJIPANGA UZINDUZI WA UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA APRILI 21, 2018

Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akisisitiza jambo

JOEL MADUKA