MWILI WA PROFESA BINAGI WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUELEKEA MKOANI MARA.

Share it:
Ndugu, jamaa na marafiki hii leo jumatano April 05,2017 wameuaga mwili wa marehemu Profesa Lloyd Manamba Binagi aliyefariki ghafla juzi jumatatu April 03,2017 Jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Mwili huo utapokelewa kesho asubuhi katika uwanja wa ndege Jijini Mwanza, na baadaye kusafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu Bomani wilayani Tarime.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika katika malalo ya Binagi yaliyopo Kenyamanyori wilayani Tarime siku ya jumapili, April 09,2017 baada ya familia ya marehemu kuwa imewasili kutoka nchini Marekani.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina!
Picha na Msubi BMG 
Share it:

JOEL MADUKA

TANZIA

Post A Comment:

Also Read

NMB YAFUNGUA MATAWI MAWILI MWANZA

Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi

JOEL MADUKA