“Niwaombe waajiri na waajiriwa kuzingatia Sheria za kazi tupunguze migogoro kazini ili tuweze kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufanya kazi” alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Ameongeza kuwa Serikali imefanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 58 ya migogoro ya kikazi inatokana na kutozingatiwa kwa taratibu za kuachishwa kazi kwa waajiriwa.
Amezitaja Sekta zinazoongoza kwa migogoro ya kazi kuwa ni Usafirishaji,ujenzi,ulinzi,binafsi,elimu,huduma za Hotel na Viwanda.
Katika kupunguza migogoro mahali pa kazi Serikali imefanya kaguzi na kusimamia uundwaji wa Mabaraza ya Wafanyakazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi imeendelea kutimiza wajibu wake wa kusuluhisha migogoro ambapo katika kipindi cha Julai hadi Februari 2016 jumla ya migogoro 8,832 ilisajiliwa na kati ya hiyo migogoro 3,319 sawa na asilimia 37.6 ya migogoro iliyosajiliwa imesuluhishwa.
Post A Comment: