MKUTANO WA MAALIM SEIF WAVAMIWA NA WATU WENYE SILAHA.

Share it:





Watu wasiofahamika wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad. 


Mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika Hoteli ya Vina, Mabibo, ulipangwa kuanza leo saa tano asubuhi lakini kabla haujaanza watu waliovalia soksi nyeusi usoni(mask) walivamia na kuanza kuwapiga wanachama wa CUF na waandishi waliokuwa kwenye mkutano huo. 


Mtu mmoja miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka. 


Mtu huyo, ambaye hajafahamika alikuwa akitoroka pamoja na wenzake katika eneo hilo la Vina Hotel Mabibo mara baada ya kutekeleza uvamizi huo katika mkutano wa wanachama wa CUF. 


Watu hao waliovamia mkutano huo, walikuwa na bastola.

Share it:

JOEL MADUKA

SIASA

Post A Comment:

Also Read

WANAFUNZI WA MADARASA YA MEMKWA,AWALI NA LA KWANZA KUNUFAIKA NA PROGRAM YA KKK GEITA.

Mwanafunzi wa darasa la MEMKWA shule ya msingi Mseto akisoma  KKK tatu darasani. Vifaa vya kujifunzia wanafun

JOEL MADUKA